Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, September 08, 2016

MBEYA; Watumishi wafukuzwa kazi

BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, wamewafukuza kazi baadhi ya watumishi kutokana na sababu mbalimbali.

Mamuzi hayo yalifikiwa katika ukumbi wa shule ya Sekondari Usongwe iliyopo ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi uliopo pembezoni mwa Jiji la Mbeya.

Kikao hicho cha madiwani kilichofanyika kwa zaidi ya saa 13, kiliwafukuza kazi Mweka hazina wa Halmashauri yao ndugu Hafidhi Mgagi, kwa kosa la Madeni ya watumishi wasio walimu.

Mtumishi huyo anatuhumiwa kutowalipa walimu hao zaidi ya Shilingi Million 115 na kwamba zilitumika katika matumizi yasiyo julikana.

Kosa lingine limetajwa kuwa ni upotevu wa pesa za Mradi wa Maji Horongo, Itimu na Mwampalala kiasi cha Shilingi Milioni 164.5 ambazo zinadaiwa kuwa zililipwa bila vielelezo vinavyo onyesha kama mkandarasi aliomba kufanya kazi hiyo. 

Mtumishi mwingine ambaye amefukuzwa ni aliyekuwa Ofisa Elimu Shule za Msingi wilayani humo Betty Laki Mlaki. ambaye anadaiwa kutoa takwimu zisizo sahihi kuhusu idadi ya madawati na upotevu wa pesa za UMITASHUMTA. 

Mtumishi wa tatu aliyefukuzwa ni aliyekuwa Ofisa Utumishi aliyetajwa kwa jina la Elissa Msana, akituhumiwa kupitisha mikataba mibovu. 

Injinia wa Halmashauri hiyo Edwini Magili, amepewa onyo kwa kosa la kusimamia vibaya mradi wa Maji na mtumishi Roveli Ng'ambi ambaye alikuwa kaimu mhandisi wa Maji ameondolewa nafasi yake ya kukaimu. 

Ofisa Habari wa Halmashauri hiyo ndugu Hamza....., amethibitisha kuwepo kwa kikao hicho na kutokea kwa maamuzi hayo ya madiwani.

No comments: