Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, September 03, 2016

MBOWE ASIWABABAISHE WATANZANIA

Mwanasheria maarufu nchini Tanzania Capt. Sambwee Shitambala, amewalalamikia waandishi wa habari kuwa wameshindwa kumhoji baadhi ya maswali ya maswali kiongozi wa kambi ya upinzani nchini hapa Freeman Mbowe kutokana na upangaji wake katika jengo la Shirika la Nyumba la nchi hiyo (NHC).

Malalamiko ya mwanasheria huyo ambaye pia ni mwanasiasa, yamekuja baada ya kusoma baadhi ya vyombo ya magazeti na mitandao ya kijamii akinukuliwa Mbowe kuwa yeye si mpangaji wa shirika hilo ambalo juzi limetoa vifaa vya makampuni yake na kuwafukuza wafanyakazi wake ikiwemo kampuni ya freemedia inayozalisha gazeti la Tanzania daima.

Mbowe ananukuliwa akisema kuwa yeye anamiliki hisa kwa asilimia 75 za nyumba hiyo palipo na ukumbi wa starehe wa Bilicanas Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Capt. Shitambala amesema kuwa, waandishi wa habari kutomuhoji baadhi ya maswali kiongozi huyo kunazua utata wa ama kutaka kumlinda ama kumweka katika ubabaishaji kiongozi huyo.

"Waandishi wa habari mnapaswa kuwa wakweli na kuwaondolea utata watanzania kwa kumwambia Mbowe kuwa kama anamiliki asilimia hizo 75 katika jengo la serikali aonyeshe mkataba" amesema Shitambala.

Ameongeza kuwa, kiongozi huyo alipewa mwezi mmoja ili alipe pesa anayodaiwa, licha ya kwamba hakwenda kulipa, lakini chama anachokiongoza Chadema, kina wanasheria wengi ambao wangeweza kwenda kuzuia mahakamani.

"Kama hata mambo ya kupikwa wanaonyesha vikaratasi kuwaaminisha watanzania, anashindwaje kuonyesha risiti za umiliki?
Kama kiongozi Mkuu wa upinzani anapaswa kuwa mfano kwa watanzania kwa kuwa mkweli na muwazi"

" Temporary court injunction au zuio la muda la mahakama. mkataba wa umiliki wake wa jengo hilo na alishindwaje kwenda mahakamani kuweka ili asifukuzwe? " alihoji mwanasheria huyo.

Amehitimisha kwa kuweka wazi kuwa naye pia ni mpangaji wa shirika hilo na hivyo Mbowe anapaswa kulipa pango na ili kutoonekana mbabaishaji atoke hadharani na kuonyesha mikataba inayomwonesha kuwa yeye ni mmiliki wa Nyumba ya serikali wakati Sheria ipo wazi na hairuhusu jambo analolisema kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni nchini humo.

No comments: