Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, September 21, 2016

MWANZA; LUMBESA BADO KIKWAZO KWA WAVUVI WA DAGAAWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.


Na Neema Joseph, Mwanza


KUTOKANA na kuwepo kwa ombwe la usimamizi wa sheria ya Vipimo hapa nchini, hivi karibuni serikali imeamua kutoa tamko la kulinda maslahi ya wauzaji wa dagaa katika masoko ya mkoa wa Mwanza.

Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitoa tamko la kukataza ujazo wa kipimo cha dagaa kwa mtindo wa  lumbesa.


“Kitendo cha wanunuzi wa mazao kushindilia magunia na kushonelea kichuguu maarufu kama lumbesa huko ni kuwaibia wakulima na kukiuka sheria”, alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

 Hata hivyo, kauli hiyo ya katazo   la   lumbesa   imekutana   na    changamoto    kubwa   kwa   upande   wa biashara   ya dagaa Jijini Mwanza,      kwani   sheria   ya vipimo  sura namba 340 ya mwaka 1982  imeshindwa  kuainisha  ujazo  rasmi wa  kutumika.


Wakazi wa Jumakisiwani kambi ya Yataka Moyo, Daudi Makunguna na Swaumu Mtanki, wanasema wananchi hawana uelewa wowote wa vipimo na kwamba agizo  la serikali bado halijatekelezwa Kisiwani hapo.


Wanasimulia kwamba wamekuwa mashuhuda wa wafanyabiashara wanaonunua dagaa  kwa kipimo cha ndoo  zilizojaa (mlima) na dagaa wengine kuanguka.

“Serikali ifike na kuangalia  namna ya kuwanusuru wavuvi na wauza Dagaa wa Jumakisiwani.” Wanaeleza wananchi hao.Takwimu za Uzito/ Tani za uvuvi  wa Dagaa kwa kipindi cha miaka sita Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Jumakisiwani Paulo Nghomele anakiri kuwepo kwa uuzwaji wa kitoweo hicho kwa mtindo wa lumbesa kwa madai kuwa wananchi hawajawahi kupata elimu juu ya kutokomeza hali hiyo.
  
"Wakala wa Vipimo wangekuwa wanatufikia wanakijiji wangekuwa na uelewa wa vipimo na wangenufaika na biashara ya dagaa tofauti na sasa" anasema Mwenyekiti huyo.


Afisa Uvuvi Mkoa wa Mwanza Titus Kilo, anasema mapato yanayotokana na uvuvi yamekuwa yakijumuishwa kwa pamoja bila kuainisha ni kiasi gani kinapatikana kutokana na dagaa.


Takwimu za uvuvi za mwaka 2010 mpaka 2015 zinaonyesha kuwa, wavuvi walipata jumla ya shilingi 261,137,759,859/= kutokana na mauzo ya tani 211,479,385 za samaki.


Licha ya baadhi ya wafanyabiashara na wananchi/wavuvi wa kisiwani kusema kuwa hawajawahi kupata elimu ya vipimo, wakala wa vipimo Mkoa wa Mwanza,  Hemed Kipengele, amesema wametekeleza agizo la serikali kwa kutoa elimu katika kanda ya ziwa mwezi Juni mwaka huu.


Ametanabaisha kwamba, katika kipindi hicho kumekuwa na uangalizi wa matumizi sahihi ya mizani  kwa kuwaeleimisha wananchi namna ya kutambua mizani zinazopima sahihi na mizani zilizochezewa ili wasiibiwe.


“Sasa hivi tunaangalia matumizi sahihi ya mizani kama zimehakikiwa na wakala wa Vipimo na kwamba kama mizani hazijahakikiwa mwaka huu utaona imewekwa alama ya ngao ya Taifa na tarakimu ya 2015”, alisema Wakala huyo wa Vipimo. 
Kwa mujibu wa taarifa ya utendaji kazi ya wakala wa Vipimo Mkoa wa Mwanza,   watu  waliokamatwa kwa kosa la kufunga  lumbesa  ni 130.

Kipengele anaeleza changamoto inayowakabili kuwa ni licha ya agizo la serikali la kukataza lumbesa kutolewa kwa vyombo vyote vya serikali lakini linaonekana kuachiwa Wakala wa Vipimo pekee.


Alivitaja vyombo vingine kuwa kwa mujibu wa barua aliyoiona kutoka TAMISEMI ni kwamba  barua hiyo ilipelekwa pia kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wakiagizwa kudhibiti lumbesa kwa kutunga kanuni ndogondogo za kutoza faini kwa watakaokamatwa na lumbesa.


Aliwataka wananchi wafuate sheria  ya vipimo ili kuondokana  na usumbufu watakaoupata na kufuata sheria na kushiriki katika mchakato wa kutunga kanuni unaofanywa na vyombo vya kutunga sheria.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema agizo la serikali juu ya lumbesa kwa ofisi yake limetekelezwa  kwa kushirikiana  na  Wakala wa Vipimo.


Alisema kwa vile wakala wa vipimo hawapo kila maeneo lakini uongozi  na mfumo wa serikali upo mpaka kwenye ngazi ya kitongoji na mtaa na kwamba katika miezi minne iliyopita kulifanyika oparesheni mkoa wote wa Mwanza.


Hata hivyo, alisema kwamba wananchi hawawezi kuendelea kufanyabiashara kwa gharama ya kujimaliza wenyewe  na kutoa mfano wa uungwana wa mshumaa kwa kuangazia watu wengine wakati wenyewe  unatekeketea.


Mongella anasema wafanyabiashara wananunua  dagaa Tanzania na kuwapeleka Kongo lakini wakifika Kigoma wanawafungua na kuwafunga upya. “sasa kwa nini Tanzania tunaweka lumbesa?”


Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umebaini kuwa, katika kijiji cha Jumakisiwani wanunuzi wa dagaa wamejipangia bei zao na kwamba muuzaji anapokataa bei zao wanagoma kununua dagaa zao na hivyo kulazimika kuuuza kwa bei za wanunuzi.


Imegundulika kwamba Serikali imeshindwa kudhibiti wafanyabiashara wa Lumbesa Vijijini bali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa maeneo ya mijini.


Hata hivyo, visiwani hakuna elimu ya ufungashaji kwa mujibu wa sheriaSerikali na hasa Wakala wa Vimipo waelekeze macho yao visiwani kwa sababu katika maeneo hayo  hakuna elimu ya ufungashaji kwa mujibu wa sheria ya vipimo.

No comments: