Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, September 27, 2016

SAUTI KUTOKA NYIKANI; Dawa za kulevya na madhara yake

Na Gordon Kalulunga, Mbeya.

Leo tuangazie dawa za kulevya aina ya Heroin ambayo inatokana na mmea unaojulikana kama Afyuni (Opium poppy).

Kilimo cha mmea huo hufanyika kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Afghanistan. Pia mmea huo unalimwa kidogo katika nchi ya Misri.

Dawa hii ya kulevya ipo katika kundi la Vipumbaza ambapo hupumbaza mfumo wa fahamu na kumsababisha mtu kusinzia, kupungua kwa mawazo na maumivu ya mwili.

Heroin huingizwa hapa nchini Tanzania kwa njia mbalimbali kama vile anga na maji ikitokea nchi za mashariki ya mbali.

Majina mengine ya Heroin ni unga, brown sugar, ngoma, ubuyu, mondo, Duke, farasi na Ponda.

Madhara yake kwa watumiaji ni kuharibika kwa mfumo wa fahamu, kupata njozi, mabadiliko ya hedhi kwa wanawake na hujenga hali ya uteja kwa haraka kuliko dawa nyingine ya kulevya.

Kwa wanaojidunga huweza kuambukizana Virusi vya Ukimwi, dozi kubwa husababisha vifo.

Ikichanganyika na pombe madhara yake ni makubwa zaidi pamoja na kifo, kizunguzungu, kichefuchefu na kufunga choo.

Kutotumia na kuacha dawa za kulevya inawezekana.

No comments: