Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, September 05, 2016

Viwanda muhimu vinavyohitajika TanzaniaViwanda vya Bidhaa za Kilimo (Agricultural Industries, including fertilizers, treatment chemicals, food processing plants, sugar, flowers, seeds and agricultural packaging, storage and transport), k.m. mafanikio makubwa ya India, China, USA, Brazil, France na Netherlands ni somo muhimu kwetu.

Viwanda vya Bidhaa za Ufugaji (Animal Industries, including animal feed, treatment chemicals, beef, dairy and poultry products, packaging, storage and transportation facilities): k.m. mafanikio makubwa ya Brazil, India, China, Australia, USA, Germany, France na Netherlands ni somo muhimu kwetu.

Viwanda vya Bidhaa za Uvuvi (Fishing Industries include activities concerned with taking, culturing, processing, preserving, storing, transporting, marketing or selling fish or fish products), k.m. mafanikio makubwa ya China, Norway, USA, India na Vietnam ni somo muhimu kwetu.

Viwanda vya madawa na vifaa vya matibabu ya binadamu.

Viwanda vya vinywaji, nguo na nyuzi, vifaa vya mawasiliano, ujenzi (k.m. saruji, bati, vigae, nondo, mabomba na misumari), usafirishaji (k.m. matairi na vipuri mbalimbali), umeme (k.m. transfoma, nyaya, mita, majiko), karatasi (na vifaa vingine vya elimu), IT, na viwanda vingine vyenye kukidhi mahitaji ya soko la ndani na la nje.


UTALII WA TANZANIA
Tanzania tutalazimika kushindana na wenzetu wa Afrika ambao wametuzidi kwa mbali sana. Mwaka 2013 Afrika ilipokea watalii zaidi ya milioni 55.7 na nchi 5 bora Afrika kwa Mwaka 2013 na idadi ya watalii waliopokelewa kwenye mabano ni:

(1)            Morocco (milioni 10), (2) Afrika Kusini (milioni 9.5), (3) Tunisia (milioni 6.2), (4) Algeria (milioni 2.7) na (5) Msumbiji (milioni 2.1, Mwaka 2012).

Nchi za Ki-Afrika zinalazimika kujipanga vizuri zaidi ili ziweze kushindana na nchi nyingine Duniani. Nchi 5 bora Duniani kwa Mwaka huo wa 2013: (1) France ilipokea watalii milioni 84.7, (2) USA milioni 69.8, (3) Spain milioni 60.7 , (4) China milioni 55.7, na (5) Italy milioni 55.7.

Umeme wa uhakika na unaotabirika; na umeme wa bei nafuu ni muhimu sana kwa uzalishaji wenye faida na ajira viwandani.

  WADHAMINI WA BLOG HII NI STEMAN ENTERPRISES

No comments: