Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, October 09, 2016

AFC ARUSHA YAANZA KUPAA...


Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Bw David Mwakiposa, amekutana na wanachama na wapenzi wa timu ya Arusha Football Club (AFC ARUSHA) katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Kutaniko hilo lilifanyika jana ambapo wanachama hao wameshukuru sana kwa kukutana na kusema kuwa hawakumbuki ni lini Viongozi wa Serikali wamewahi kukaa nao kujadili changamoto zao kwa pamoja.

Akiwa anafungua kikao hicho Mwakiposa aliwaambia wanachama kuwa anaamini kero walizonazo si zote zinahitaji fedha. Hivyo akaweleza wawe huru kuzungumza kwa uwazi kwani tunataka kupata mwarobaini ili Arusha ndani ya muda fupi ianze kupaa ktk medani ya michezno kitaifa na kimataifa kwani hili ni jiji la kimataifa.. Kikao hicho kilidumu kwa masaa karibu manne.

 Ajenda kuu ilikuwa kujadili AFC ilikotoka ilipo sasa na inakokwenda. Ubadhirifu, ubabaishaji, kuendekeza siasa na fitina vilitajwa kuwa moja ya vikwazo vikubwa kwa kufanikiwa kwa timu hiyo. 

Baada ya mjadala wa muda mrefu maazimio yalifikiwa ya kutengua uongozi uliokuwepo kwani kwanza haukuwa wa kidemokrasia pili umeonakana  kulega lega katika kusukuna gurudumu hili.  Imeundwa Kamati ya watu 7( Care Taker Committee) ikiwa na jukumu moja tu kuivusha timu ligi hii na kisha uchaguzi utafanyika.

 Wapenzi wa mpira na wanachama wameonyesha furaha isiyo kifani na kushukuru sana Setikali kwa kuwathamini na kunuia kufufua Michezo Arusha.


 Akizungumza wakati wa kufunga Kikao hicho Katibu Tawala huyo aliwaambia wanachama na wapenzi kuwa jukumu la kwanza lililo mbele yatu ni kuisafisha timu dhidi ya matope ya ufisadi ili iweze kuamainika tena. Wakae cjini walete mapendekezo jumatatu ili Serikali ianze kufanyia kazibharaka Sana. 

Hata hivyo  amewaonya kuwa kiongozi yeyote atakayeelekea kuwa mbadhirifu afahamu kuwa mkono wa serikali utamfikia na hatabaki salama. Aliwaeleza wajumbe kuwa haiwezekani Tanga, Mbeya ambazo hazina wadau wengi wala potentials wengi ukilinganisha na Arusha iwe na timu zinazoshiriki ligi Kuu lakini Arusha timu zote nne yaani MADINI,PEPSI,AFC&OLJORO ziwe daraja la nne. Hili halikubaliki mbinguni wala.duniani.

Akakawaambia pia kuwa wasitegemee kuchangisha michango kwa wadau wkati wao wenye timu hawajatoa hata shs kumi ndipo ikaanza "toa ndugu toa ukichonacho" ilifanyika harambee hapo na zikaptikana Cash zaidi ya 150,000, dola za kimarekani na ahadi zaidi laki nane. Wanachama wamekubaliana week ijayo wakutane wadau wengi kuvhangishana kabla hawajaenda kwenye makampuni kuomba udhamini.
 Wanachama na wapenzi wa soka mjini Arusha wakimsikiliza Mwakiposa hapo jana.

Chanzo; Saul Mwaisenye

No comments: