Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, October 04, 2016

MICHEZO; Tujifunze kutoka kwa Maradona


Na MosesNg’wat,Mbeya.

KATIKA Falsafa ya mchezo wa mpira wa miguu au kama wenginewanavyoweza kuita kabumbu au majina mengine mengi unayoyajua, mkono unahesabikakama ni shetani wa mchezo huo.

Basi kama lilivyo jina la mchezo wenyewe, yaani mpira wamiguu, mchezaji haruhusiwi kutumia mkono bali golikipa pekee ndiye anaruhusa yakutumia mkono. 

Hata hivyo, golikipa anaruhusiwa kutumia mikono yake katikaeneo dogo tu la uwanja lisilozidi yadi 18 kati ya yadi 110 za eneo linalotumikakuchezea mchezo huo (Pitch). Kimsingi nje ya eneo hilo golikipa naye haruhusiwi kutumiamikono bali ni miguu ili kusaidia timu yake isipate madhara.

Mazingira ya kuutawala mchezo huu wa mpira wa miguuyamewekwa vizuri sana kwa kutumia sheria 17 na kanuni zake, mfano mpiraunaotoka nje ya eneo la kuchezea au kwa lugha rahisi ukitoka nje ya uwanjahurudishwa uwanjani kwa mkono. 

Lakini wachezaji walio ndani hawaruhusiwi kuupokea kwa mkonotena huo mpira unaorudishwa uwanjani baada ya kutoka eneo la kuchezea, balihupokelewa kwa mguu ili kuendelea kutafuta mbinu za kupata matokeo yaanikufunga mabao. Hivyo basi wachezaji wanaruhusiwa kutumia sehemu nyingineyeyote ya miili yao kama kichwa, kidevu, tumbo, kisigino, kidevu hata mgongo,lakini kamwe si mkono.

Kutumia mkono hasa kwa kudhamiria au makusudi ni dhambikubwa ambayo haisameheki katika soka  naadhabu yake mara nyingi ni kubaguliwa(kutolewa nje) katika mchezo huo tena kwakadi nyekundu kuashiria wewe ni mtu hatari na hufai kuendelea kushiriki mchezohuo uletao burudani isiyoisha utamu. 

Kutokana na mazingira hayo, hakika mkono ni shetani  mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu na niwapefaraja wapenzi, mashabiki na wanazi wa klabu ya Simba kuwa si wao pekeewalioumizwa na tukio la kisanaa lililofanywa na Amis Tambwe kwa mwamuzi MartinSanya. 

Kwanini nasema tukio la kisanaa, mchezo wa soka au mpira wamiguu ni sanaa kama ilivyo sanaa nyingine hivyo uwasilishaji wake kwa hadhiraunaweza kutawaliwa na matukio ya asili au ya kutengeneza. 

Hali hiyo pia hutawaliwa sana na imani kwa hiyo likitokeatukio lisilo la kawaida katika kuaminisha linaweza kuibua mijadala mizito,lakini mwisho wa siku tukio hilo linabaki kuwa katika kumbukumbu bila kujalinzuri au mbaya. 

kwa falsafa hiyo, basi kumbe mchezaji unaweza kutumia sanaaili kuficha uhalisia au kumhadaa anayekusimamia ilimradi upate matokeo na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mchezaji AmisTambwe katika dakika ya 26 ya mchezo huo.

 Licha ya hali hiyo iliibua hisia mbaya kwa mashabiki waSimba na kuanza vurugu kwa kubandua na kuharibu viti vya uwanja wa Taifa ambaoumejengwa kwa gharama kubwa  inayotokanana fedha za walipa kodi, wakiwemo wao wenyewe. Nawasihi wakubaliane na hali hiyo na kukubali matokeo ilimwisho tuendelee na kusonga mbele badala ya kuendelea kunyosheana vidole .

Kwa kifupi tuu, kuna matukio mengi ya namna hiyo katikaulimwengu wa sokaambayo yamebaki kuwa kumbukumbu mbaya ya kuumiza kwa upande mmoja, ilhali kwa upande wa pili nifuraha zisizofutika katika meneo yao au mataifa yao. 

Kuna mifano mingi duniani iliyoibua tafrani kubwa kutokanana kama kile kilichotokea katika mchezo wa mwisho wa wiki kati ya Yanga naSimba katika uwanja wa Taifa, ambapo mashabiki wa samba walikosa uvumilivu nakufanya uharibifu mkubwa. 

June 13 mwaka huu timu ya Taifa ya Brazili iliondolewakwenye mashindano ya Copa America baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Peru, baolilozua tafrani kubwa baada ya mfungaji wake Raul Ruidiaz kudaiwa kufunga kwamkono. 

Mchezo huo ulisimama kwa dakika kumi wachezaji wa braziliwakimlaumu mwamuzi kuwa mfungaji alitumia dhambi ya kushika kwa mkono kabla yakufunga bao, lakini hakika mwamuzi hakufanikiwa kubaini sanaa iliyotumiwa namfungaji wa bao hilo alilikubali na kuwang’oa Brazili katika mashindanomakubwa. 

Mfano mwingine ambao kama nisingeutoa hapa watu wangiwangeweza kinishangaa basi ni lile tukio la kihistolia la gwiji wa soka dunianiDiego Maradona.

 Ilikuwa katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1986 kuleMexco  katika pambano kati ya Argentinaya Maradona na Uingereza ambapo Maradona aliweka historia ya kipekee katikaulimwengu wa soka kwa kufunga bao la mkono. 

Bao hilo lilizua balaa kubwa, lakini kitu pekee ni pale baohilo lilipo batizwa jina la bao la mkono wa mungu, najua kwa waingereza hii nimbaya kuliko katika historia yao ya mchezo wa mpira wa miguu licha ya kwamba waondio waanzilishi wa mchezo huu mwaka 1908. 

Lakini nilikwambia mwanzo kuwa soka ni sanaa kama zilivyosanaa nyingine tu, inategemea mhusika anaiwasilishaje kwani katika pambano hilolicha ya Maradona kulaumiwa kwa usanii wake wa bao la mkono wa mungu.

 Ikiwa ni muda mfupi baada ya kufunga bao hilo, alidhihirishakuwa yeye ni msanii na anaijua kazi yake, baaba ya kufanya maajabu mengine kwakuwalamba chenga karibu nusu ya walinzi wa timu ya Taifa ya Uingireza nakufunga bao lingine zuri. 

Kimsingi hapa Maradona alitaka kutufundisha kuwa kwenye sokaunaweza kutumia sanaa kadiri uwezavyo ilimradi upate matokeo bora tena bilakuathiri sheria na kanuni, ndio maana baada ya kulaumiwa kwa bao la mkono mudamfupi akafunga bao la mguu na kuonesha umahiri wa uwasilishaji wa sanaa.

Kwa mara nyingine nirudie tena kwa mashabiki wa Simba nasoka kwa ujumla matokeo ya uwanjani yatategemea zaidi mazingira na namnawahusika walivyojiandaa kwa uwasilishaji wake bila kuvunja sheria na kanu zake. 

Pamoja na mambo yote naomba nitoe tahadhari kuwa , simatukio yote yanayofanana na lile la Tambwe yanaweza yakawa yametokea tu kwauhalisia wake, bali tunaomba wahusika wote wanaosimamia mchezo wajitathimini nakuwa wakweli katika uendeshaji wa mchezo wenyewe.

 Mwandishi anapatikana kwa simu namba 0752-25 64 99

No comments: