Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, October 07, 2016

MBARALI; Wakamatwa kwa tuhuma za kufuja fedha za Kijiji

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

Viongozi wanane wa kijiji cha Kapunga Kata ya Itamboleo Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutuhumiwa kutafuna fedha za serikali ya kijiji  zaidi ya shilingi milioni 18.

Akitoa agizo hilo mbele ya  mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kapunga mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Mfune kuwa hayupo tayari kufumbia macho ufujwaji wa mali ya umma  katika Wilaya ya Mbarali.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali Ezekiel Kilemile amewataja waliokamatwa kuwa ni Brighton Mwinuka ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji, Selemani Mwakanyamale Mwenyekiti  wa kamati ya Fedha, Rhoida Pole Mtunza Hazina na Geophrey Mwinuka.

Wengine ni Zamda Nyani,Joseph Mwinuka, Siliko Mwinuka na Peter Kita aliyekuwa mtendaji Kata ya Itamboleo. Aidha Mkuu wa Wilaya ameagiza kufanyika kwa uchunguzi juu ya waliohusika na uuzwaji wa mashamba na viwanja katika kijiji cha Kapunga mara baada ya Serikali kurejesha eneo la Kapunga lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji lililorejeshwa January 4 mwaka huu na waziri wa ardhi William Lukuvi.

Pia amesema kuwa mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji cha Kapunga na Ukwavila pande mbili hizo zikutane ili kumaliza mgogoro huo na kufikia maridhiano kwa kuwatumia wazee wa pande hizo mbili.

No comments: