Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, October 04, 2016

TFDA; Kuweni makini na bidhaa za viwandani  Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda Rodney Alananga akifafanua jambo wakati wa semina iliyowahusisha wanahabari 120 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.(Picha na Rashid Mkwinda)

*Wananchi waonywa kuepuka bidhaa za kitapeli
*Wanadanganywa kuna sabuni za kurejesha bikira

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

WATANZANIA wametakiwa kuwa makini katika utambuzi wa bidhaa za viwandani hasa zinazozalishwa hapa nchini kwa kuwa imegundulika baadhi hazina ubora.

Tahadhari hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kanda ya Nyanda za juu kusini, Rodney Alananga, katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake Jijini Mbeya.

Amesema siku za hivi karibuni kumetokea utapeli wa baadhi ya wazalishaji wa bidhaa zikiwemo sabuni ambazo zimekuwa zikitangazwa na kuandikwa kwenye vifungashio kuwa zinarudisha usichana (bikra) kwa wanawake, jambo ambalo si kweli.
“Kuna wazalishaji wasio wakweli, wanaandika kwenye vifungashio vya sabuni kuwa sabuni zao zinarudisha bikra kwa wanawake, jambo ambalo sayansi inakataa na hata wakiulizwa mchanganyiko wa vitu walivyochanganya na vipimo vyake ndani ya sabuni hizo wanashindwa kujieleza” alisema Alananga.

Meneja huyo alisema, kutokana na mamlaka yake kugundua uwepo wa bidhaa hizo sokoni, mwaka 2013-2014 waliandaa mafunzo ya kanuni ya bora za uzalishaji na ufungashaji kwa wazalishaji 76 mkoani Mbeya lakini mrejesho umekuwa mdogo wa kuhitaji kusajiliwa bidhaa zao katika mamlaka hiyo.

“Wananchi wanaponunua bidhaa yeyote ya kiwandani wawe makini na kuangalia kama bidhaa hiyo ina jina halisi la biashara, tarehe iliyozalishwa bidhaa hiyo, na tarehe ya mwisho ya matumizi, mahali ilipotengenezwa, muhusika aliyetengeneza na mawasiliano ya mtengenezaji,” alifafanua Meneja huyo.

Alisema kwa kufanya hivyo ni haki ya mteja na ni matakwa ya kisheria kuhakikisha vitu hivyo vinakuwepo kwenye vifungashio.

Alipoulizwa kwa nini tahadhari hiyo inatolewa, alisema upotoshaji wa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye vifungashio umeleta changamoto kubwa kwa walaji na kwamba TFDA imebaini kuwa katika viwanda vingi vidogo vidogo ndiko kwenye changamoto nyingi kuliko viwanda vikubwa.

“Tunaendelea kufanya ukaguzi madukani na kwenye viwanda vidogo vidogo kwasababu wengi wanazalisha katika mazingira ambayo sheria hairuhusu kutokana na uchafu uliokithiri ikiwemo vifaa vya kuzalishia, usafi binafsi mfano, ukataji wa kucha, upimaji wa afya, kukohoa nk” alisema Alananga.

Alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wawekezaji wadogo kujiunga pamoja na kwamba ni vema watafute eneo la kujenga viwanda na TFDA itawashauri jinsi ya  kujengaviwanda hivyo urahisi wa kusajili bidhaa zao. Wametakiwa watumie fursa iliyotolewa na Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene ya kuiagiza kila Halmashauri nchini kutenga maeneo ya kilimo na uwekezaji wa Viwanda.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipokuwa akifunga maonyesho ya wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale mwaka huu mkoani Mbeya, alisema aliliridhishwa na usindikaji wa vyakula ambavyo alivikuta alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho hayo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, vyakula hivyo ambavyo alivisifia katika hotuba yake, vingi havijasajiliwa na TFDA.

“Nilipopita katika mabanda, nimekuta vyakula mbalimbali vilivyosagwa kwa ubora ambao unaweza kuleta tija kwa watoto wetu wa umri wa miaka mitano na uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. serikali yetu imedhamiria kuyapa mazao haya kuyapa thamani kubwa ili kuweka msisitizo wa ujenzi wa viwanda nchini.”
“Agizo hili ni la kitaifa, Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya wote katika ukanda huu wa Nyanda za kusini na kwa taifa lote kwa ujumla, tumesisitiza kuwa tutenge maeneo ya uwekezaji, tukaribishe wawekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vinavyoweza kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa lengo la kuyapa thamani.” Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

No comments: