Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, October 05, 2016

VIWANDA; Wananchi watoa tahadhali kwa Magufuli

*Mkuu wa wilaya naye aeleza fedha zilivyo kikwazo

Na Gordon Kalulunga

Wakati kiwanda cha NMC Iringa kikiwa tayari kimefufuliwa chini ya Bodi ya nafaka mchanganyiko (CPB), baadhi ya wananchi wanatabiri kuwa hakitadumu bali kiwanda hicho na vingine vya umma vitakufa kama ilivyotokea miaka ya 1990 kote nchini na kwamba vitakavyonusurika ni vile vya watu binafsi.

Hayo yameelezwa baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa ambapo wamesema kuwa hata kufufuliwa kwa kiwanda cha kusaga unga NMC Iringa bado hawajaona manufaa yake kwao.

Mbali na uongozi wa kiwanda hicho kusema kuwa wananunua mahindi kutoka kwa wakulima, baadhi ya wakulima wamesema kuwa jambo hilo si sahihi na kwamba wakuima wanachokifahamu ni kwamba mahindi yanayosagwa kiwandani hapo yanatoka katika Hifadhi ya taifa ya chakula iliyopo Makambako mkoa wa Njombe.

Mwananchi Anna Sekalinga, anasema haoni faida ya kiwanda hicho kwa jamii inayokizunguka bali anaona kimefufuliwa kwasababu za kisiasa tu.

Naye Mariam Mkolwe anasema hata ajira hawajaziona na hakigusi maisha yao moja kwa moja.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alipoulizwa kuhusu manufaa ya kufufuliwa kwa kiwanda hicho kwa wananchi alisema kuwa wakulima wataongeza kipato kupitia mazao yao hasa Mahindi na kwamba ajira za vibarua pia zitaongezeka.

“Pia maghala yaliyo jengwa na halmashauri yatatumika ipasavyo
Ismani, kihorogota , Itunundu, idodi na nina kata 28 vijiji 133 iringa
DC, Manispaa kata 18,” alisema Kasesela.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema changamoto kubwa ni mtaji mdogo Kwa kiwanda inayowafanya wawe na hofu ya kuhamasisha wakulima.

“Bodi haina fedha nyingi kununua mazao. Bodi iruhusiwe kuuza bidhaa hii nje ya nchi mfano malawi, Zimbabwe nk nchi hizi zina uhaba wa chakula kwa kufanya hivyo mtaji utaongezeka. Wakulima wana mazao mengi hawana pa kuyauza” alieleza Mkuu huyo wa wilaya.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa, Shirika la hifadhi la taifa NSSF
linatarajia kutoa mtaji kwenye bodi ya mazao mchanganyiko kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda hicho mtaji ili kiweze kununua mazao kutoka kwa wakulima wa kanda ya Nyanda za juu kusini.

No comments: