Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, November 30, 2016

RC MAKALLA AAGIZA WAKURUGENZI KUTENGA MAENEO NA FEFHA MIKOPO KWA VIJANA


- Awataka Vijana kutambua fursa katika maeneo yao na kuzitumia.

- Alipongeza shirika la Technoserve kwa kutoa Mafunzo YA ujasiriamali.
.....................................................................................................
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amewaagiza wakurugenzi wa HALMASHAURI zote Mkoa wa Mbeya kutenga maeneo kwa ajili YA wajasiriamali wakiwemo Vijana ili wafanye biashara na viwanda vidogo vidogo.

Hayo ameyasema leo wakati akifunga Mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana 1,811 kutoka jiji la Mbeya na Wilaya ya Rungwe Mafunzo yaliyo ratifies na shirika la Techoserve.

Aidha amewataka kutenga Fedha kupitia mapato ya ndani na kutoa mikopo nafuu kwa Vijana na wanawake kwa kufanya hivyo itasaidia Makundi hayo kuanzisha au kukuza biashara zao .

Amewataka Vijana kutobweteka badala yake wajishughulishe na kutumia fursa zilizopo ktk jamii  kujipatia kipato.

Amesema hakuna serikali itakayokuja na kuwafuata vijiweni ili iwapatie Fedha bali atahahakikisha maeneo ya kufanyia biashara au kilimo wanawapatia Vijana wenye kuhitaji na sambamba na hilo HALMASHAURI zitenge Fedha kwa ajili ya mikopo ya riba nafuu

No comments: