Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, November 17, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.11.2016.


Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, Operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata hivyo kumekuwa na tukio 01 la mauaji kama ifuatavyo:-Mnamo tarehe 15.12.2016 majira ya saa 03:00 usiku huko katika maeneo ya Mlima Reli, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Bonde la Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la ISAMBI YELA (36) Mkazi wa Mwashiwawala alikutwa ameuawa kwa kukatwa kichwa na miguu na mtu/watu wasiofahamika.Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa kuwa ni tuhuma za wizi baada ya marehemu kukutwa amevunja nyumba mali ya PETER EDWIN (40) Mkazi wa Mlima Reli Mbalizi kwa nia ya kuiba.Aidha katika tukio hilo, mwili wa marehemu ulikutwa hauna ubongo, baadhi ya meno yakiwa yameng’olewa, jicho la kushoto limetolewa na mguu wa kulia ukiwa umekatwa na kuvunjwa.Mtuhumiwa mmoja amekamatwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hili ambaye ni PETER EDWIN ambaye nae alikutwa na majeraha sehemu ya mdomoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.WITO:Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa kwa yeyote mwenye taarifa za mtu/watu waliohusika katika tukio la kikatili kutoa taarifa ya siri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao. Aidha anatoa wito kwa wananchi kuacha kutafuta mali kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato na sio kujihusisha na uhalifu.
                                                

Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


No comments: