Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, December 31, 2016

FIKRA ANGAVU: WEWE NI SHUJAA

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

Leo Jumamosi ya Desemba 31, 2016 tunakunja jamvi la mwaka 2016 kuelekea mwaka 2017.

Kuna waliokusema sana kwa mabaya, kukusingizia, kukudharau, kukusengenya, kukutakia mabaya, kukusudia kukuchafua ili ukose heshima na mambo kadha wa kadha, lakini Mungu ameendelea kukuinua na laana kuwarejeshea wao maana wewe ni shujaa.

Umeugua sana na baadhi wakatamani ufe bila kujua kuwa Mungu anafanya ukarabati wa mwili wako ili uimarike zaidi, wakajifanya kukuzidi madarasa basi wao ni bora kuliko wewe lakini Mungu akaendelea kukupa heshima kuu katika mioyo ya watu walio wengi na wakawapuuza vikaragosi hao maana walikuwa hawajui kuwa wewe ni shujaa, sasa unapaswa kuinuka na kujitwika godoro lako na kuenda.

Tia bidii katika ukifanyacho na ongeza maarifa na ubunifu utaendelea kufanikiwa.

Mwaka 2017 ndoto yako inaenda kutimia kwa kusigina Nyoka na Nge huku Mungu akipigana na watesi wako maana wewe ni shujaa.

Watesi wako wanaenda kuaibika zaidi na hawatakufa mpaka watakaposhuhudia ukifanikiwa na kumtukuza Mungu huku ukihudumia watu.

Wakijaribu kukimbilia hata Baharini, bahari itawakimbia maana uwepo wa Mungu ndani yako ni mkubwa kuliko wanavyodhani, maana wewe ni shujaa.

Mwaka 2017 usitamani kupanda cheo au kupandishwa mshahara bali tamani kuongeza wigo wa mahusiano na kuwahudumia watu, hapo utapata mafanikio kuliko hata bosi wako maana ukuu wa Mungu utakujilia wewe usiye na mawaa kwa kuwa sasa unaenda kuwa mkuu wa mashujaa na Mungu anaenda kukuhekimisha zaidi..

Wenye mawaa na wewe ukikutana nao wataanza kutabasamu kinafiki mbele yako kwasababu ushujaa wako wa kuhimili hila zao uliupuuza 2016 na kutosadiki moyoni mwako maana wewe umeteuliwa kuwa shujaa.

Katika ushujaa wako usilipize kisasi bali achilia Moyo wako uwe mweupe na muombe Mungu uwe na moyo wa msamaha na kutupilia mbali hasira za ziada.

Tambua kuwa mna hila nyingi moyoni mwa mwanadamu, hivyo Mimi my friend wako nakutuma muda huu wakati ukijiandaa kuupokea mwaka mpya 2017, jitambue kuwa wewe ni sawa na Kondoo kati kati ya Mbwa mwitu.

Wanaokusema na kukufanyia ubaya na kutamani udhalilike au ufedheheke ni wachache kuliko wanaokuwazia mema hivyo songa mbele, wapuuze mara elfu maana wewe ni shujaa.

 Katika maisha tunatakiwa tuwe kama noti ya shilingi elfu kumi hata ikifinyangwa bado thamani yake inakuwa ni ile ile.

Katika maisha kuna kipindi utasalitiwa, utakanyagwa, utaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee.

Kiri sasa kwa kinywa chako kwa kusema mimi ni shujaa, kisha shusha pumzi. Songa mbele maana wewe ni shujaa.

Ni mimi my friend wako, Gordon Kalulunga.
0754 440 749 kalulunga2006@gmailcom
WEB; www.kalulunga.blogspot.com

No comments: