Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, December 08, 2016

WALIOMVAMIA MFIKEMO WAFUNGWA JELA

Na  Ezekiel Kamanga, Mbeya

Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela na faini ya shilingi milioni moja na laki moja kila mmoja ndugu watano wa familia moja kwa makosa mawili ya kujeruhi watu wawili wa familia moja Lwitiko Osiah Mwandemele na mwanawe Ambilike Lwitiko .

Hakimu wa Mahakama ya mkoa Venance John Mlingi baada amesema kesi hiyo namba CC 118 inayowakabili ndugu watano wa familia moja kwa makosa ya kujeruhi ni pamoja na Fredy Osiah Mwandemele, Alinine Osiah Mwandemele, Kairo Osiah Mwandemele, Livingstone Osiah Mwandemele na Richard Osiah Mwandemele ambao kwa pamoja waliwashambulia Lwitiko Osiah Mwandemele na Ambilike Lwitiko juni 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika kitongoji cha Vingunguti Kata ya Isyesye Jijini Mbeya mbele ya Afisa Mtendaji wa mtaa Mariam Ngole na mafundi na kuwasababishia majeraha.

Hakimu Mlingi amesema washitakiwa wote watano wamekutwa na hatia katika makosa mawili moja ni la kumjeruhi vibaya Lwitiko Osiah Mwandemele kinyume cha sheria namba 225/16/2002 na kosa la pili kumjeruhi kidogo Ambilike Lwitiko kinyume cha sheria namba 228(a)/16/2002.

Wakili Mwandamizi Catherine Gwaltu ambaye aliwakilishwa na wakili Heberi Kihaka ambaye aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wanaojichukulia sheria mkononi na kwamba uhalifu haulipi.Aidha baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili imewatia hatiani kwenda jela miaka saba kutokana na makosa yote mawili .

Hakimu Mlingi amesema washitakiwa wote watano ni ndugu na majeruhi wote ni ndugu hivyo jambo hilo ni aibu kwa jamii inayowazunguka kwani kama kulikuwa na tofauti walikuwa na nafasi ya kuzungumza na si kujichukulia sheria mkononi kama walivyofanya. Upande wa mashitaka ulileta mashahidi tisa na washitakiwa walikuwa na mashahidi kumi hivyo mahakama ilikubaliana na ushahidi upande wa mashitaka hasa Mtendaji, Madaktari, Mafundi na vielelezo kama PF 3 ambazo zilipokelewa kama vielelezo.

Aidha aliwataka washitakiwa kujitetea ambapo kwa pamoja waliiomba mahakama kuwahurumia kwa kuwa wana familia kuwa zinawategemea pia wao ni ndugu wa familia moja hivyo wanaomba adhabu ndogo kwani wamejifunza kupitia tatizo hilo na kwamba hawakuwa na nia mbaya.

Akisoma hukumu iliyochukua saa 2:20 kuanzia saa 8:30 mchana Hakimu Mlingi alizingatia utetezi wa washitakiwa hivyo aliwahukumu kwenda jela miaka miwili na miezi sita na fidia ya milioni moja kila mmoja kwa kosa la kumjeruhi Lwitiko Osiah Mwandemele na shilingi laki moja kila mmoja kwa kosa la kumjeruhi Ambilike na Adhabu zote zitakwenda kwa pamoja.

Nje ya mahakama vilio na simanzi vilitawala kwa wake na watoto wa ndugu watano ambao wakipanda gari la Polisi tayari kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.

No comments: