Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, December 10, 2016

POLISI WAVAA VIATU VYA KIKE UGANDA KUTETEA WANAWAKEMaafisa kadha wa polisi wa kiume nchini Uganda leo walivalia viatu vya kike na kushiriki katika matembezi kwa lengo la kuhamasisha jamii dhidi ya udhalilishaji na dhuluma dhidi ya wanawake.

Polisi hao walikuwa wanashiriki katika matembezi yafahamikayo kama 'Walk A Mile in Her Shoes' (Tembea Maili Moja na Kiatu Chake).

Pichani ni baadhi ya maafisa waliovalia viatu hivyo zimesambazwa sana mtandaoni.

Polisi hao waliandaa matembezi hayo kwa ushirikiano na mashirika ya kutetea haki za wanawake.
Shirika la Walk A Mile in Her Shoes linaloandaa matembezi hayo lilianzishwa mwaka 2001 na Frank Baird. Lilianza kama kundi la wanawake waliokuwa wakijitokeza na kutembea kwenye bustani wakiwa wamevalia viatu vya wanawake.

Lakini sasa limekuwa shirika kubwa na kila mwaka maelfu ya watu hushiriki kuchangisha pesa za kusaidia vituo vinavyowasaidia waathiriwa wa ubakaji, waathiriwa wa dhuluma nyumbani pamoja na miradi inayokabiliana au kupinga dhuluma na unyanyasaji wa wanawake.

Chanzo;bbc swahili

No comments: