Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, December 05, 2016

RAIS MAGUFULI ONA MAITI HIZI 22 ZA WAJAWAZITO

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo tena nimeona nikuandikie waraka huu mfupi sana kutoka huku Nyikani.
Nafahamu una majukumu mengi sana ya kitaifa lakini pia nafahamu kuwa urais ni taasisi hivyo hata hili nalo linakuhusu.

Kuna majanga yametangazwa nchini kuwa majanga ya kitaifa ukiwemo UKIMWI, lakini kuna janga kubwa lingine.

Nahisi ndege zinazobeba abiria watano zingepata ajali ndege NNE au Tano na kuua abiria wote kila siku ingetangazwa kuwa janga la kitaifa.

Mheshimiwa Rais, takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wanawake 22-34 wanafariki nchini kwetu kila siku kutokana na matatizo ya uzazi.

Takwimu hizo watu wa Nyikani zinatuliza sana na tunafananisha na ajali za ndege tano za abiria ambazo zingekuwa zinaua abiria kila siku. Litazame hilo.

Mheshimiwa Rais, mbali na vifo hivyo vya wanawake, nchi yetu Tanzania kila mwaka watoto wachanga 39,000 hawaishi zaidi ya mwezi mmoja wa maisha yao.

Tunashika nafasi ya 11 miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga ulimwenguni.

Vifo vingi vya watoto wachanga hutokea katika kipindi cha kuzaliwa -kipindi ambacho hatua madhubuti za kuokoa maisha yao zinanahitajika.

Hivi sasa vifo vya watoto wachanga vinachangia asilimia 40 ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano.

Na zaidi ya hapo watoto wachanga 46,000 huzaliwa wafu-karibu nusu yao wanakufa wakiwa wanazaliwa.

Uhai wa watoto wachanga zaidi ya asilimia 80 ya vifo vyote vya watoto wachanga kutokana na sababu zinazozuilika.

Maisha ya watoto hao yangeweza kuokolewa kwa kuwepo dawa na huduma zingine rahisi.

Huduma za kuokoa maisha ya mtoto mchanga ikiwemo kumsaidia kupumua. Utunzaji (usafi) wa kitovu chake. Viua vijidudu (Antibiotiki). Huduma ya ngozi kwa ngozi (Kangaroo) mama na mtoto mchanga.

Pia unyonyeshaji maziwa ya mama. Kuwa na Wahudumu wa Afya wenye ujuzi.

Msisitizo ukiwekwa katika SAA 48 baada ya kujifungua.

Mheshimiwa Rais, ni hayo tu kwa leo ambayo yanasababisha mashavu yangu kulowa machozi huku kwikwi isiyokatika ikiwa katika koo langu ikiwalilia wanawake na watoto wanaokufa kila mawio na machweo.

Ni mimi Gordon Kalulunga wa Fikra Angavu kutoka huku Nyikani.

SIMU; 0754 440 749
EMAIL; kalulunga2006@gmail.com

No comments: