Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, December 16, 2016

TANZANIA; MWANZILISHI WA JAMII FORUMS MAXENCE MELO, AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU
NEWS ALERT: Mwanzilishi wa JamiiForums Maxence Melo, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar leo
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

 Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums Maxence Melo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka matatu.


Maxence amesomewa shtaka la kwanza na la pili chini ya hakimu mfawidhi  Victoria Nongwa, Kosa la kwanza ni kuzuia na kuharibu data ambazo jeshi la Polisi wamekuwa wakizihitaji kwa ajili ya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Cyber Act. Kosa la pili ni kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya makosa ya mtandaoni.


Baada ya kusomewa Mashtaka mawili,mshtakiwa akahamishiwa chumba kingine cha Mahakama ambako alisomewa Kosa la tatu,Mbele ya Hakimu mkazi, Godfrey Mwambapa.Kosa hilo ni la kumiliki 'Website' ambayo haina Domain ya Tanzania kinyume na kifungu cha 7 cha sheria ya EPOCA.Mshtakiwa alifanikiwa kupata dhamana ya makosa mawili. 


Hata hivyo Maxence alirudishwa mahabusu mara baada ya taratibu za dhamana katika kosa la tatu kushindwa kukamilika kutokana na mmoja wa wadhamini kutokuwa na barua inayomtambulisha kwa hakimu kutoka taasisi anayofanyia kazi. Hata alipofanikiwa kufanya hivyo muda wa mahakama uikuwa umekwisha.


Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akiongozwa na Askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo, kusomewa mashtaka yanayomkabili kama inavyosomeka hapa chini> (Chanzo;Michuzi blog)

No comments: