Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, January 18, 2017

AFARIKI MUDA MFUPI BAADA YA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

Na Ezekiel Kamanga, Chunya

Godfrey Elikana(31)mkazi wa MatundasiWulaya ya Chunya Mkoani Mbeya amefariki dunia muda mfupi baada ya kuhumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya Wilaya ya Chunya.

Kesi iliendeshwa na Hakimu mfawidhi wa Wilaya ya Chunya Mheshimiwa Osmund Ngatunga alimkuta mshitakiwa na hatia ya kumlawiti mtoto jinsi ya kike  mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Matundasi na kumsababishia maumivu mahali.

Siku ya hukumu Januari 17 mwaka huu mara baada ya kutuhumiwa alipelekwa mahabusu ya Polisi Chunya akisubiri kupelekwa Gereza la Ruanda Mbeya saa Mbili asubuhi januari 18 mwaka huu kwa kuwa Wilaya ya Chunya haina Gereza la wafungwa .

Marehemu akijitetea mbele ya Mahakama aliomba mahakama imuonee huruma kwa anaumwa ugonjwa wa ukimwi sababu ambayo mahakama haikukubaliana nayo na hivyo kumhukumu kifungo cha maisha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Emmanuel Lukula amesema marehemu akifikishwa mahabusu majira ya alasili baada ya kutoka mahamani ambapo usiku alianza kutetemeka kwa baridi hali ilipozidi kuwa mbaya alikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Chunya ambapo amefariki alfajiri saa 11 januari 18 mwaka huu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Wilaya kusubiri ndugu kwa ajili ya  taratibu za mazishi.

No comments: