Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, January 11, 2017

DC CHUNYA AKAGUA VYOO KWA KUSHTUKIZA

Katika kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya hawakumbwi na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na ukosefu wa vyoo mkuu wa Wilaya hiyo Rehema Madusa ameanza ziara ya kushitukiza katika Kata mbalimbali ili kufanya ukaguzi wa vyoo kaya na Taasisi za serikali na dini zina vyoo vya kisasa .

Madusa amesema kuwa lengo la ziara yake ni kuhimiza kila mwananchi anakuwa na choo ili kuepukana na magonjwa ya kipindupindu au yanayotokana na mkojo.

Hivi karibuni mkuu wa Wilaya amefanya ziara katika Kata ya Chokaa na Sangambi vijiji vya Shoga,Igundu, Godima na kujionea kaya nyingi na Taasisi  ambazo hazina vyoo hivyo kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa.

 Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amehimiza wananchi kukamilisha ujenzi wa madarasa mapya, nyumba za walimu na Zahanati ili kuondoa adha kwa wananchi ambapo ametoa miezi miwili kukamilika kwa majengo katika vijiji alivyotembelea.

Ametoa mwezi mmoja kwa kila kaya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuwa na choo na atakayekiuka anakabiliwa na faini ya shilingi laki mbili au kifungo Gerezani.

Madusa amesema hatakuwa tayari kuona mwananchi wa Wilaya ya Chunya anakufa kwa magonjwa yanayoweza kuepukika.

No comments: