Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

FIKRA ANGAVU; 2017 TUCHAGUANE BILA KUWABUGUDHI WENYE UALBINO


Na Gordon Kalulunga

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Chama Cha Mapinduzi kitaanza chaguzi zake za jumuiya mwezi wa sita mwaka huu.

Vyama vingine bado dawati la watu wa nyikani halijapokea kuwa wataanza lini.

Katika Lugha ya kiswahili kuna maneno watatu yanayotoa maana tofauti likiwemo neno Zamani, Zama na Enzi.

Nikianza na neno Zama. Zama ni kipindi maalum kinachofafanua mazingira fulani na teknolojia fulani mfano zama za mawe, zama za chuma.

Zamani linamaanisha kipindi kilichopita, hivyo neno zama na zamani havina uhusiano .

Neno Enzi kuna kumuenzi mtu au kuelezea nyakati.

Msomaji wangu leo nitaelezea tukio linalohusisha neno zamani, yaani tukio (matukio) yaliyowahi kutokea hasa vipindi vya chaguzi za serikali ama vyama vya siasa.

Historia hainyamazi kuhusu mauaji ya watu wanaoishi na upungufu wa rangi nyeusi katika miili yao, yaani wenye ualbino.

Tumukuwa tukisikia sana vipindi vya miaka ya uchaguzi wanadamu hawa wakiuawa, kuteswa na hata kukatwa viungo vyao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, askari wa jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Mbalizi Mbeya vijijini na wananchi wa kitongoji cha Songambele kijiji cha Mumba kata ya Masoko walishuhudia tukio baya la watu kufukua mwili wa aliyekuwa na ualbino.

Tukio hilo lilibainika majira ya saa Tatu usiku tarehe 3.01.2017 hadi mchana wa Tarehe 4.01.2017 kwa kupambana na watu waliokuwa wanafukua kaburi la marehemu Sista Sisala Simwali mtu mwenye Ualbino aliyefariki tarehe 28/2/2008 na kuzikwa tarehe 29/2/2008 kwenye makaburi ya familia hiyo baada ya kuugua homa.

Watu wawili walikamatwa katika tukio hilo kati yao mmoja alikufa kwenye eneo la tukio baada ya wananchi kupandwa na hasira Kali.

Tukio hilo lilivuta hisia kwa wananchi wa kata za Masoko, Ilembo na Shizuvi waliofurika kwa wingi kwenye eneo la tukio.

Taarifa za mahusiano ya chaguzi za serikali, vyama vya siasa na mauaji ya watu wenye ualbino hazipaswi kupuuzwa. Ndiyo maana nasema 2017 tuchaguane bila kuwabugudhi wenye Ualbino.

Mwandishi wa Makala hii ya uchambuzi anapatikana kwa simu
0754 440 749
Email; kalulunga2006@gmail.com

No comments: