Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, January 30, 2017

HIVI NDIVYO MWENYEKITI WA CCM MBEYA ALIVYOPIGWA RISASI

 Mwenyekiti was CCM wilaya ya Mbeya mjini ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitality ya Rufaa Mbeya asubuhi ya leo.

Na Veronica Chonde, Mbeya

*Alidhani ni mlipuko wa simu ya kiganjani
*Tukio lahusishwa na migogoro ya ardhi


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbeya mjini Ephrahim Mwaitenda, ambaye asubuhi ya leo mtandao huu wa Kalulunga blog ulikuwa wa kwanza kuripoti taarifa zake, anaendelea vizuri baada ya kupigwa risasi mgongoni na watu wasiojulikana akiwa wilayani Kyela mkoani hapa ambako ni nyumbani kwao.Tukio hilo limetokea leo majira ya saa saba usiku wa kuamkia Januari 30 mwaka huu katika kijiji cha Makwale Kata ya Makwale wilayani humo mkoani hapa.Baada ya kupokelewa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Mwenyekiti huyo alisema majira ya usiku alihisi kama kuna vishindo nje ya nyumba aliyokuwa amelala ambapo alilazimika kuamka na kuanza kusali.“Nilipomaliza kusali huku nikiwa na simu yangu ya kiganjani kando ya kitanda changu nikasikia sauti ya mlipuko na kudhani ni simu yangu imenilipukia, ndipo nikatoa sauti ya kuomba msaada” alisema Mwaitenda.Alisema baada ya ndugu zake na majirani kuamka waliingia chumbani na kukagua simu ambayo waliikuta ikiwa salama bali kioo cha chumbani kikiwa kimepasuka huku damu zikiwa zinamvuja.Mkurugenzi wa Hospitali ya rufaa ya Mbeya Fred Mbwanji, alithibitisha kumpokea kiongozi huyo majira ya saa mbili asubuhi na kwamba madaktari walimpa matibabu ya awali na kuendelea kumtibu kwa kumpeleka katika chumba cha upigaji picha (Ex ray), ili kubaini zilipo risasi.“Nilishiriki kumpokea asubuhi ambapo anasema alipigwa risasi majira ya saa saba huko wilayani Kyela na majeraha aliyopata ni mgongoni upande wa bega la kulia na sasa anaendelea vizuri chini ya madaktari bingwa” alisema Dr. Mbwanji.Kwa upande wake Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Zongo Lobe Zongo, alisema wanalaani tukio hilo na kwamba wanaamini vyombo vya dola vitatimiza wajibu wao kwa kuwatia nguvuni waliohusika na tukio hilo.“Tulipata taarifa majira ya saa saba na nusu usiku kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Ntinika ndipo tukaendelea kufanya mawasiliano ambapo saa tisa usiku askari polisi wilayani Kyela walifanikiwa kwenda kumchukua majeruhi na asubuhi ya leo saa mbili na nusu tumempokea hapa Rufaa” alisema Zongo.Aliwaomba wanafamilia kuwa watulivu huku akisema vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya chini ya Mkuu wa Mkoa Amosi Makalla anaamini vitafanya kazi yake na kwamba tangu walipopata taarifa za tukio hilo Mkuu huyo wa Mkoa yupo bega kwa bega nao.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia tukio hilo na kama kuna watu waliokatwa, simu zake hazikuweza kupatikana na tulipomtafuta kwa simu ya ofisini alipokea ofisa mmoja huku akitutaka tupige simu namba 0658376006 ambayo iliita kwa mara kadhaa lakini haikupokelewa.

Hata hivyo, kikosi kazi cha blog hii kinaendelea kuujua ukweli zaidi wa tukio hilo ambapo kesho tutakuletea habari zaidi. Endelea kuwa nasi wakati wote.


Kulia ni kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika Hospitali ya rufaa Mbeya asubuhi ya leo.

No comments: