Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

MAHUSIANO; MAMBO AMBAYO UNATAKIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA

Pastor, Gordon Kalulunga.


MOJA ya mambo ambayo yanakosekana katika nyumba za ibada ni mafundisho ya mahusiano.
Watu wengi hawajui kuwa mtu aliyeolewa na hajaolewa au kuoa, ana haki ya kupata elimu ya ndoa.
Unaweza kujiuliza kuwa kwanini ndoa nyingi zina shida? Jawabu ni kwamba wengi wanajua ndoa baada ya kuingia kwenye ndoa, hawajawahi kupata elimu ya mahusiano.
Ni sawa na kumfundisha dereva kuendesha gari.
Wengi wamekosa elimu ya mahusiano au kuoa au kuolewa, vijana na mahusiano, bali wengi wana elimu za upako wa mafanikio na toa ndugu toa ndugu ndiyo masomo tuliyoyazoea.
Mfumo wa elimu tuliyonayo nao ni tatizo. Kwa mfano kwenye Biblia hakuna neno linalosema rafiki au mchumba.
Huwezi kukuta kitu kinachoitwa, urafiki, uchumba baadaye ndoa.
Ngoja nikuambie, Mathayo Mtakatifu sura ya 1;1-23. Mariamu alipoposwa….. haisemi alichumbiwa! Lakini katika utamaduni wa kimagharibi leo hii watu wanasema kuwa mchumba wa Yusufu.
Mchumba huwa anapimwa, ndiyo maana watu wanakuwa na wachumba wengi kweli na hatimaye uchumba unavunjika kwasababu hakuna mtu anayeenea kwenye utimilifu.
Kuna fix za kifikra ambazo zina ugonjwa wa kufisha, kesho unaweza kulia ukiendekeza kumtafuta mchumba badala ya kumtafuta mume au mke.
Akina dada wengi wanaomba na kusugua magoti wakiomba wapate wachumba.
Maandiko yanasema kuwa, ‘’Mjibu mpumbavu kutokana na upumbavu wake’’
Mtu ana wachumba kadhaa, kisha anaanza kumuomba Mungu ampe mume au mke huku akiwa na vinyago vyake. Majibu yatakuja kama anavyowaza. 
Yaani tayari wana fikra, vinyago na maamuzi yao kati ya wale wachumba waliopo moyoni na kichwani.
Mungu atamjibu mtu kutokana na elimu aliyonayo ya urafiki, uchumba kisha ndoa.
 Walio kwenye ndoa wengi wanajuta kwasababu wameoa au kuolewa na rafiki….
Ukikaa na mtu utasikia anakuambia, mtumishi nimeumia, tunakuabudu Bwana, utafikiri upako umetembea, kumbe watu wana kesi zao na nafsi zao zimepigwa.
Mimi kama mwalimu ambaye sawa na Daktari, nikianza kufuatilia ninajua.
Ukimuuliza vipi ina maana una chimichimi ya roho mtakatifu ndiyo maana kila tunapoanza kuabudu analia?
Ukidadisi mtu anakumbia kuwa, nilikuwa na mchumba akaniambia utanioa, akamwambia na rafiki yangu na mwingine…..
Nafsi za watu wa Mungu nyingi zimeumizwa na kuna kesi nyingi za kuachwa kuliko kesi za uhalifu mwingine.
Ukiomba mchumba, wanaweza kuja wengi kisha unapoanza kuburuzana nao unachoka kisha unatumbukia popote…..
Jambo hili la ndoa na uchumba ni gumu kwasababu vijana wengi ni wavivu kujifunza maandiko ya Mungu bali wanataka watafuniwe kila kitu na kulishwa.
Mungu ni roho, alimuumba mtu kwa mfano wake, akasema nendeni duniani mkazae na kuongezeka. Maandiko yanaposema Mtu, ina maanisha mfano wa roho.
Kwenye ulimwengu wa roho, Mungu aliumba mtu mke na mtu mume na ndiyo maana amekataza kuzini.
Maana yake ni kwamba kila mmoja ana mke wake na ana mume wake kwasababu kila mmoja aliumbwa na wake.
Ukiishika elimu hiyo, hautalia kwasababu eti hujapata mume au mke. Mbinguni kuna roho nyingi zinazataka kuja duniani, hivyo tuliopo tumepata neema ya kutangulia kuzaliwa.
Unapomuona mwanaume anapita, ujue kuwa huyo ni mume wa mtu na mwanake anayepita ni mke wa mtu.
Tatizo watu wanaomba kwa Mungu wapate mke au mume huku wakilia! Inashangaza mtu unaenda kudai deni lako huku akilia. Maana yake hajui haki yake, yaani imani zetu hazijawa sawa.
Kama ndani yako una usongo wa kuoa au kuolewa, fanya hivi. Kwa imani nenda kamnunulie na suti iweke ndani maana kwa imani yupo. Acha kushika yeyote mwisho utashika hata majoka.
Mungu hupendezwa na mtu mwenye imani na anamletea. Acha kulia.
Wanaume ngoja niwaambie. Mungu alipokuwa akiumba, alimtanguliza Brother men, kisha akamlaza usingizi na kuchomoa ubavu akamtengeneza mwanamke. Maana yake ni kwamba mwanamke wa kwako yupo, labda uwe towashi.
Wanawake hampaswi kufifia ngozi kwamba hamtaolewa, maana usigeweza kuumbwa bila wa kwako kuwepo na wala hajafa bali yupo, cha kufanya amini. Kanunue na suti kaweke ndani, anza kufanya maandalizi…
Kuweni na imani inayowekwa kwenye matendo, msiamni kuwa mtakosea.
Sehemu nyingine huwa nawafundisha kuwa, ukishatambua kuwa wa kwako yupo, tulia au subiri.
Kwa kuwa hatuamini kuwa wa kwako yupo, hatutulii, na kwa kuwa tunaanza kaba ya majira na wakati ndipo tunapoeekea kwenye kuumia na majuto ya uchumba na ndoa.
Wimbo uiobora 3;5 ….msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha……Mungu anasema hayo kwasababu kabla ya Mungu kuyaamsha, wewe unawahi.
Mfano; Sekondari mtu hasa wanawake, anapokuwa kidato cha pili tu au kabla ya hapo, anaanza kuomba, Mungu nipe Mume….. hebu jiulize wewe ulianza lini kuzitikisa mbingu za mapenzi…… jibu unalo.
Wanyakyusa wanao usemi kwa mtu mzima anayefanya mambo ya hovyo, unasema…..amakambo, akwesile ndili… yaani mtu huyo anasumbuliwa na bangi….alivuta lini?
Hapa namaanisha kuwa unaweza kukimbilia na ukapata mume maana hakuna mtu anayekuwa anazijua tabia za wenzake, kisha utaanza kusema kuwa aaaaa…kumbe hakuwa mwenyewe..
Ibrahimu haraka zake zinasumbua kule Israel mpaka leo. 
Niwaambie ukweli kuwa haraka zina hasara zake sawa na utunzaji wa mtoto njiti ni kazi kubwa. Hivyo ukiharakisha unaweza kupata mume au mke njiti…
Sijui kama ninaeleweka katika somo hili. Haraka zinaendana na akina dada kuongea harakaharaka, wanaume wengi hawapendi mwanamke wa namna hiyo.
Yesu aliwahi kujaribiwa na kahaba, mafarisayo miili yao ikawa nyang’anyang’a huku yule kahaba akitoa machozi na kufuta miguu ya Yesu kwa nywele zake, hivi ungekuwa wewe Brother men ungefanyaje hapo?
Usiwe na haraka. Watoto wa kike ndo wana speed kuliko hata dunia inavyozunguka jua.
Hamnoni alimpenda Tamali mpaka akaumwa…. Lakini baada ya kulala naye akamchukia na kumwambia Tamali aondoke na akamchukia kwelikweli…..tafakari.
Hapa kinachotendeka katika ulimwengu wa roho ni kependa umbo lakini my akionja hakuti kile ambacho alikuwa anakifikiri.
Mfano mzuri ni kwamba wanaume na wanawake wengi ambao wamedumu katika mapenzi hawaoani.
Mwanaume akitembea na mwanamke na kutokukuta alichokitarajia, anasema hata kwa wenzake kuwa ‘’demu mwenyewe mshamba na hana lolote’’ yote hiyo ni kuyachochea mapema na kuvua. 
Nitajuaje kama ndiye?
Kimaandiko unapomuomba Mungu, utawekewa rohoni kitu kinachoitwa mwongozo.
Utaona unasukumwa na jambo la kuolewa kama kuku navyosumbuka kutafuta eneo la kutagia, sawa na mtumishi wa Mungu anapotaka kufanya jambo la kiroho.
Jifunze kumsikiliza Mungu, ondoa moyoni kufikiri kuwa huyo unayefikiri na kumweka moyoni kama ni mwenyewe, huyo siyo. Achana naye maana roho ya mauti ipo juu yako. Tubu.  
MSIKILIZE MUNGU ILI ASIKUJIBU SAWA SAWA NA VINYAGO ULIVYOWEKA MOYONI MWAKO NA KUJIINGIZA POPOTE. 
HEBU JIULIZE, MPAKA SASA UNA VINYAGO VINGAPI?

Mungu awabariki na awasamehe wote wenye toba.


Gordon Kalulunga
Information and Media Consultant
P.O. Box 705, Mbeya-Tanzania
Tel: 255 (0)754 440749
WEB; www.kalulunga.blogspot.com

No comments: