Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

MAJI KIKWAZO KWA WAKAZI MUHEZANa Gordon Kalulunga, Tanga

WANAWAKE wa Vijiji vya Kwabada kata ya Kwabada na Kibaoni kata ya Mtindilo wilayani Muheza mkoani Tanga, wameiomba serikali kupeleka miundombinu ya maji katika Vijiji hivyo ili kuwaondolea adha ya maji iliyopo sasa.

Wakizungumza na Mwandishi wa habari hii katika vijiji hivyo, walisema kuwa kwa sasa wanatumia maji ya visima katika kupikia na kunywa.

“tunashukuru nasi tumetembelewa nawe Mwandishi huku vijijini. Maji yenyewe hayo tunayapata kwa kuyanunua kwa baadhi ya watu wenye uwezo ambapo kila ndoo yenye ujazo wa lita 20 huwa tunanunua Tsh. 150-Tsh. 200” alisema Tumaini Mtega, mkazi wa kijiji cha Kwabada.

Alieleza kwamba, mwaka jana 2015 wananchi walihamasishwa kuchimba mitaro kisha mabomba yakatandazwa lakini mpaka sasa hawajaona maji ya Bomba.

Naye Amida Suleiman mkazi wa kijiji cha Kibaoni alisema kwamba, kuna mahala inafikia kwa watu ambao wanahitaji maji safi ya bomba wanalazimika kukodi pikipiki kwa Tsh. 5,000/= kwenda Muheza mjini ambako lita 20 za maji uuzwa Tsh.100/=. Soma zaidi kwa kubofya link ifuatayo.

Wakati adha hiyo ikiwapata wananchi hao, katika eneo la Lewa Kibaoni ndani ya kata ya Kwabada, kuna bwawa la maji ambayo yanaweza kuhudumia wananchi wa kata hizo mbili endapo serikali itaamua kulitumia kama chanzo cha maji ya bomba.

No comments: