Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, January 03, 2017

MALIGHAFI ‘zinazobakwa’ ZINAKWAMISHA VIWANDA BORANa Gordon KalulungaUVUNAJI wa malighafi za kilimo ambazo hazijakomaa maarufu kama ‘kuzibaka’, zimetajwa kuwa moja ya kikwazo katika kufikia malengo ya viwanda vya ndani.Hayo yamebainishwa na wasindikaji na wakufunzi wa masuala ya usindikaji nchini kupitia SIDO Mbeya, Rehema Msina na Anitha Mwasajone.Wakizungumza katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hii katika maonyesho ya wajasiriamali wadogo wa kanda ya Nyanda za juu Kusini, yaliyofanyika hivi karibuni katika bustani ya jiji la Mbeya walisema kuna malighafi nyingi zipo sokoni ambazo zimevunwa kabla ya kukomaa hivyo zikisindikwa bidhaa haziwi bora.Walizitaja baadhi ya bidhaa hizo ambazo zinaongoza ‘kubakwa’ kuwa ni pamoja na nyanya, karanga, maembe na machungwa.Changamoto zingine za kukuza na uanzishwaji wa viwanda vya ndani hasa viwanda vidogo walisema ni pamoja na mlundikano wa kodi ambazo ni upimaji wa ubora wa bidhaa moja katika mamlaka zaidi ya moja ikiwemo TBS na TFDA, usalama wa jengo OSHA, Leseni ya biashara Halmashauri, Zima moto na kulipia upimwaji wa bidhaa zao kwa dola za kimarekani ambazo hufikia kiasi cha Shilingi 600,000 TFD tu.“Nafuu TBS wanapima bidhaa zetu kwa Tsh 50,000 tofauti na hawa TFDA ambao sisi tayari tumepata vibali vyao lakini baada ya kupitia changamoto mbalimbali ikiwemo uchelewashaji wa upimaji bidhaa huku mitaji ikiwa ni moja ya kikwazo kikubwa kwa wajasiriamali. Pia kuhusu kuwa na jengo kwa mjasiriamali ni kazi kubwa kwasababu wengi ni wapangaji” walisema wajasiriamali hao ambao wapo eneo la Nane Nanye Uyole.Aidha, walieleza kuwa changamoto nyingine itokanayo na mikopo ni wajasiriamali kutoaminiana na kwa upande wa serikali hasa mikopo ya vijana na wanawake kutoka katika Halmashauri na utengwaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanda vidogo utekelezwaji wake ni hafifu.Kuhusu ubora wa Malighafi wanasema kuna tatizo kubwa katika kuelekea mafanikio ya biashara za wa wajasiriamali ambao wanategemea malighafi za hapa nchini kwasababu wakulima wengi wanatumia mbolea na madawa ambayo bidhaa zikipimwa kimataifa hukosa ubora huku ubora wa vifungashio nao ukiwa unatia shaka na hapa TBS ikilaumiwa kuwa wanaruhusu vifungashio kuingizwa nchini ambavyo baadhi vinakuwa chini ya ubora.

No comments: