Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

MITAMBO ILIVYOODOLEWA New Mbeya Textile
NA GORDON KALULUNGA

Moja ya chanzo cha kuuawa kiwanda cha New Mbeya Texitile Ltd kilichopo Mbeya Vijijini, kimetajwa kuwa ni kutokana na ung’oaji wa mitambo ya kiwanda hicho tangu mwaka 2003.

Taarifa zinasema kuwa, moja ya mtambo ambao ulikuwa ukitumika kuzalishia vitenge bora ndani ya kiwanda hicho uliondolewa kufuatia kutiwa sahihi mkataba na pande mbili za wawekezaji wa kiwanda cha New Mbeya Textile Mill Ltd na Mwatex (2001).

Mtambo huo uliondolewa katika kiwanda cha New Mbeya Textile Mill Ltd kisha kusafirishwa April 24, 2003 kwa gari kubwa lenye namba za usajili TZ 68933/TZE 5862.

kwa mujibu wa barua hiyo ambayo ilitoka katika uongozi wa New Mbeya Textile Mill Limited, Songwe Industrial Area yenye kichwa cha habari kisemacho, TO WHOMSOEVER IT MAY CONCERN inasema “As per the agreement dated 27th March 2003 between M/s. New Mbeya Textile Mill Ltd., P.O. Box. 950, Mbeya, Tanzania and M/s Mwatex (2001) Ltd., P.O. Box 1420, Mwanza, Tanzania, we are sending herewith the used Printing Machinery parts and accessories to M/s Mwatex (2001) Ltd. Through Truck No. Tz 68933 / TZE 5862.
We hereby declare that there is no sale involved in this transaction” imeeleza barua hiyo.


Mitambo mingine ambayo ‘iling’olewa’

Mitambo mingine ambayo inadaiwa kuondolewa kinyemelea ndani ya kiwanda hicho ni pamoja na mitambo 8 iliyokuwepo eneo la kupokea pamba Blow room, Cabing machines 8, mtambo mmoja uliokuwa unatumika kupima ubora wa nyuzi eneo la Labaroatory, mtambo wa kusafisha nyuzi, mitambo 780 iliyokuwa ikitumika kusokota nyuzi ambayo ilitoka nchini Polland, mitambo 8 ya kuhakiki nguo nayo haipo huku eneo la mitambo hiyo ikigeuzwa eneo la kuhifadhia tumbaku na kuchakata chini ya kampuni iitwayo Premmierm Tanzania Ltd na mitambo ya zana zingine zikiwemo za kuchonga vifaa vya viwandani (Workshop tolls).


Aidha taarifa za uhakika kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho tangu mwaka 1999, zimesema kuwa mbali na mitambo hiyo, kuna mtambo mwingine mpya wa kuzalishia vitenge bora ambao ulitoka nchini Ujerumani na kuhifadhiwa katika ghala maarufu kama Cotton back stoo, nao uliondolewa na mwekezaji huyo kwa kushirikiana na aliyekuwa fundi umeme wa kiwanda hicho aliyejulikana kwa jina la Abed.

“Ilituuma sana lakini hatukuwa na namna ya kufanya maana mtambo huo uliondolewa na gari moja aina ya Scania pamoja na motor zaidi ya 26 ambazo kila mota moja ilikuwa na thamani ya kuanzia Milioni nane mpaka Milioni 20” walisema wafanyakazi hao ambao waliomba hifadhi ya majina yao.
 

Naye aliyekuwa karani wa mahesabu wa kiwanda hicho Asajile Kandonga (64), anasema yeye ni mmoja wa wafanyakazi wa kwanza katika kiwanda hicho ambapo Januri 15 mwaka 1999 ndipo ukarabati wa kiwanda hicho ulianza na majaribio ya uzalishaji walianza Agosti 2, 1999 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2000.

Ushahidi zaidi watamalaki
Karani huyo wa mahesabu ambaye anasema pia ni mtaalam wa vipuli vya viwandani, alisema yeye ni shahidi muhimu wa utoroshwaji wa mitambo ya kiwanda hicho ambapo aliwahi kuhusika kukamata magari yaliyokuwa yakitorosha mitambo hiyo na kuifikisha katika kituo kikuu cha Polisi mkoa wa Mbeya, lakini baadae mitambo hiyo ikatoroshwa ikiwa chini ya ulinzi wa polisi.

“Mwekezaji amehujumu kiwanda lakini serikali inaendelea kubembelezana naye. Mwaka 2002 Printa yenye thamani ya zaidi ya Milioni 98 iliibiwa na kupakiwa kwenye Scania. Mwaka 2012 malori yakaanza kusomba mitambo mingine, tukaenda kufunga makufuli getini, baadae wakaja OCD Mbeya na RAS wakiwa na askari”…

“Wakatuuliza kuna nini, tukawajibu kuwa kuna wizi wa mitambo, hatukujali kama tungeweza hata kuuawa kwa risasi, baadae RAS na OCD wakaenda pembeni kuzungumza na wakarejea tulipokuwa kisha wakasema tuachie, tukakataa mpaka pale gari ilipofikishwa kituoni na tulienda watu kumi na kutoa maelezo kwa maadishi lakini hatukujua kuwa OCD alikuwa na mipango ya pamoja na mwekezaji, gari ikatoroshwa” alisema Kandonga.

Mbali na hayo, anathibitisha kuwa aliyekuwa fundi umeme aliyemtaja kwa jina la Abel, pia alikuwa akitumika katika wizi wa mitambo hiyo kwa kushirikiana na mwekezaji ambapo aliwahi kuhusika katika utoroshwaji wa mitambo ya ku-control umeme wa mitambo (Contol Pannel).

Ukwepaji wa kodi ulivyofanywa

Kandonga anaeleza kuwa, katika kipindi chote cha uzalishaji wa Kanga na vitenge katika kiwanda hicho, mwekezaji alikuwa anahujumu uchumi wa nchi kwa kukwepa kodi ambapo mbinu iliyokuwa ikitumika ni kuwa na vitabu viwili vya utoaji wa mzigo getini.

“Kulikuwa na meneja mwenye asili ya kiasia aliyeitwa Kontianka ambaye alikuwa akiaminiwa sana na Mkurugenzi wa Kiwanda ambapo alikuwa anatuamuru kupunguza asilimia 25 za mahesabu huku wakifika getini nako walikuwa wakionyesha karatasi ya bello 600, lakini magari yakitoa nje tukagundua kuwa walikuwa na vitabu vingine ambavyo vilikuwa vinaonyesha kuwa mzigo uliopakiwa ni bello za nguo mita 300 tu ambazo ndizo zilikuwa zikisomeka na serikalini” alisema karani huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa New Mbeya Textile Mill Ltd, Barakat Ladhan alipotafutwa kwa njia ya simu na hata kuandikiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yke ya kiganjani, hajaweza kutoa majibu yeyote.

Kuhojiwa na Tume

Mfanyakazi huyo wa zamani wa kiwanda hicho, anakiri kuwa tayari tume iliyoundwa na serikali ikihusisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutaka kuujua ukweli wa wizi unaodhaniwa kufanywa na mwekezaji wa kiwanda hicho, tayari imemuhoji na ameieleza ukweli wote ikiwa ni pamoja na ushahidi wa anayoyafahamu.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala alipoulizwa kuhusu uundwaji wa tume na majibu yake alisema serikali tayari imeanza kuchukua hatua.

“Kwa ufupi serikali ya mkoa imeshachukua hatua na tunawasiliana na msajili wa hazina kwa hatua zaidi” alisema Makalla.

Taarifa za kufungwa kiwanda hicho mwaka 2011 kutoka kwa mwekezaji huyo zilidai kuwa ni kutokana na ukosefu wa zao la Pamba kutoka wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, lakini cha kushangaza badala ya kununua zao hilo kutoka mkoani Tabora na Mwanza, mitambo ikaanza kuuzwa wakati taarifa zinasema mkataba wa mauziano unamtaka Mwekezaji kama ameshindwa kuendesha kiwanda alipaswa kukirejesha serikalini.

Nguo zilizokuwa zikizalishwa katika kiwanda cha New Mbeya Texitile Mill Ltd, zilikuwa na soko kubwa ndani ya nchi na katika masoko ya Lubumbashi nchini DRC Congo na Kamwala Market Lusaka nchini Zambia.

No comments: