Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

MLINZI NMC: SERIKALI INASHAWISHI WATANZANIA KUWA MAFISADI*Wamelinda kiwanda tangu mwaka 1987
*Walishawishika kuuza mitambo waliukataa
*Sasa wamesimamishwa kazi bila barua

N a Gordon Kalulunga

WALIOKUWA walinzi wa Kiwanda cha kusaga unga National Millingi Coparation (NMC) cha mjini Iringa, wamesema kuwa Serikali inajenga mfumo wa wananchi kuwa mafisadi.

Walinzi hao ambao kwa sasa wanasema wanapata kiongeza machozi badala ya kifuta machozi, waliyasema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hizi, baada ya kupata taarifa zao za uaminifu katika kazi ya ulinzi wa kiwanda hicho tangu mwaka 1987 mpaka mwaka jana 2015 ambapo kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa unga wa Mahindi chini ya Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko (CPB), lakini hawajalipwa mafao yao.

Mlinzi Hussein Sokela, alisema kuwa baada ya shirika la NMC kusitisha uzalishaji miaka ya 1990, wao kama walinzi waliendelea kukilinda kiwanda hicho na kutunza mitambo iliyopo huku wakifanyia usafi mitambo hiyo.

Alisema changamoto kubwa waliyokuwa wakikabiliana nayo ni vishawishi kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho kabla hakijasimama kuzalisha, ambao walikuwa wakiwaendea kuwashawishi ili waingie ndani ya Kiwanda na Kung’oa baadhi ya mashine, lakini wao waliweka msimamo na kuwakatalia.

“Tumefanya kazi katika mazingira magumu sana na kwa uaminifu mkubwa, lakini ajabu mpaka uzee huu, wanatuzungusha kutupatia mafao yetu, nchi hii kumbe bora kuwa fisadi kuliko kuwa mwaminifu…”.

“Mitambo ipo salama kwa nguvu zetu na mpaka akina Zitto Kabwe walipokuja hapa walisema tunapaswa hata kupelekwa bungeni kutambulishwa kwa uzalendo wetu” alisema Sokella.

Kwa upande wake aliyekuwa mlinzi mkuu wa Kiwanda hicho Ignas Mbughi (71), mbali na kulalamikia kusumbuliwa kupatiwa mafao yao, alisema katika ulinzi wa mitambo ya kiwanda hicho walikuwa wanatumia mbinu zao, ambazo hakutaka kuzitaja.

Alipoulizwa silaha ambazo walikuwa wakitumia za kisasa, alitanabaisha kwamba katika kiwanda hicho kulikuwa na silaha moja aina ya Gobole ambayo hakuwahi kuwa na risasi hivyo uaminifu na uzalendo ndiyo ilikuwa silaha yao kuu.

“Tumesumbuka sana na wezi kutoka nje ya Kiwanda lakini na baadhi ya walinzi ambao walikuwa wanakuja kujumuika nasi huku wakiwa na dhamira mbaya ya kutaka kuiba, nilikuwa nawafukuza na wezi wan je tulikuwa tukiwakamata tukawa tunawapeleka Polisi na kuwaacha huko” alisema Mbughi.

Mkuu huyo wa ulinzi wa kiwanda hicho cha NMC, alisema kwa sasa kutokana na umri wake aliacha kulinda na mpaka sasa anaendelea kusubiri mafao yake ambayo uongozi wa Kiwanda umewaambia kuwa wanaandaa mafao hayo na kwamba hivi karibuni Waziri wa Ajira, Jenista Muhagama alipotembelea kiwandani hapo na wao wakasikia na kumpelekea malalamiko yao.

Baadhi ya walinzi ambao wanadai mafao yao katika kiwanda hicho ni Ignasi Mbughi, John Bosco, Hessein Sokella na Bruno Lyelu.

No comments: