Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 15, 2017

MWEKEZAJI APINGWA KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA
 Na Gordon Kalulunga, Mbeya

Diwani wa kata ya Bonde la Songwe, Ayas Njarambaha mahala ambapo ndipo kilipo kiwanda cha New Mbeya textile Mill Ltd, kilichokuwa kikizalisha nguo, amepinga uamuzi wa Mwekezaji wa Kiwanda hicho kubadili matumizi na kutaka kusagisha unga wa sembe.

Ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao huu ambapo amesema “Hii haijakaa vizuri hata kidogo, mwekezaji anasema anataka kubadili matumizi ya kiwanda cha nguo kwa kisingizio kuwa pamba iliyokuwa ikilimwa Chunya haipatikani, sasa watueleze kuwa je kiwanda cha Urafiki Dar es Salaam. Pamba inalimwa Kibaha? Alihoji diwani huyo.

Naye Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa, alipohojiwa kuhusu sababu za kufungwa kiwanda hicho kama anazifahamu ni nini maoni yake kuhusu kiwanda hicho kubadilishwa matumizi alisema hapo ni muhimu msajili wa hazina aeleze makataba ukoje maana miundombinu ilijengwa kwa ajili ya kiwanda cha nguo.

“Dar es Salaam kuna viwanda vya nguo lakini hakuna mashamba ya Pamba. Nimewahi kuhoji sababu zilizopelekea kiwanda hicho kufa nikaambiwa ni ukosefu wa Pmaba na mdudu mwekundu, sasa je hao watafiti tangu walifanya utafiti na kugundua kuwa kuna mdudu huyo na hatimaye kiwanda kikafa, kwanini hawajafanya utafiti mwingine wa jinsi ya kumuua huyo mdudu? alihoji Dkt. Mary Mwanjelwa.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Oran Njeza, naye alipohijiwa swali hilo hilo alisema “Yote yanategemea mkataba wa ubinafsishaji na mwongozo anao msajili wa hazina. Kinachohitajika ni kipi katika mipango mikakati 2 ina faida kwa wananchi na taifa letu” imesomeka sms yake ambayo alijibu swali la mwandishi kwa njia ya mtandao wa Whats App.

Kiwanda hicho kilikuwa kikiajiri wafanyakazi 600, lakini taarifa zinasema kuwa endapo mwekezaji huyo atabadili matumizi na kuanza kusagisha unga wa Sembe, kitaweza kuajiri wafanyakazi 200.

No comments: