Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, January 11, 2017

MWIMBAJI AMANI MWASOTE AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Kesi namba CC 168 inayomkabili Mwinjilisti na Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Amani Mwasote imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya.

Mahakama hiyo imemuona Amani Mwasote ana kesi ya kujibu ambapo imedaiwa kuwa Mwasote akiwa Mhubiri katika mkutano wa Injili September 20 mwaka jana alimtaja binti mwenye umri wa miaka tisa kuwa ni mchawi.

Wakili wa Serikali katika kesi hiyo Heberi Kihaka ambaye alikamilisha kwa kuleta mashahidi kadhaa mbele ya Hakimu Venance John Mlingi ambapo mahakama ilimuona Amani ana kesi ya kujibu hivyo kutakiwa kuanza kujitetea ambapo aliongozwa na wakili wa utetezi Sambwee Shitambala.

Akimuongoza mtuhumiwa Amani Mwasote alikanusha kumwita mtoto huyo ni mchawi bali mtoto huyo alikumbwa na pepo hivyo alifika katika mkutano huo kwa maombezi kama walivyofanya watu mbalimbali wakubwa kwa wadogo.

Upande wa utetezi ulileta mashahidi wawili ambao ni walimu wa Amani Mwasote katika chuo cha Biblia Kalobe. Baada ya mashahidi hao upande wa utetezi kumaliza utetezi na upande wa mashitaka Hakimu Venance John Mlingi aliahirisha kesi hadi February 6 mwaka huu mahakama itakapotoa hukumu.

Mlingi aliesema dhamana kwa mtuhumiwa inaendelea.

No comments: