Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, January 31, 2017

RC MAKALLA AUSITILI MLIMA MBEYA,*MAMLAKA YA MAJI SAFI NA TAKA YAIOMBA SERIKALI KULIPA ANKARA ZA MAJI

 MBEYA

KUFUATIA mambo kutokwenda vizuri katika kuuhifadhi mlima Mbeya uliopo kusini mwa Tanzania tangu mwaka 1957, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makalla, leo ameongoza wananchi na watumishi wa idara mbalimbali za serikali kupanda miti, chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.

Akihutubia wananchi walioshiriki upandaji miti hiyo ikiwa ni kilele cha kampeni za upandani miti kimkoa katika safu za mlima huo ambao ni chanzo kikuu cha Maji cha mito na vijito vinavyonufaisha Wilaya za Mbeya, Chunya na Mbarali Mbeya na Wilaya ya Songwe mkoa wa Songwe, alisikitishwa na uchomaji moto, kilimo, ufugaji na ukataji wa miti unaofanywa katika mlima huo.

“Pia nimearifiwa kuwa lengo la mwaka huu ni kupanda miti 120,000 yaani miti rafiki kwenye vyanzo vya maji 80,000 ya Matunda na kivuli 25,000 na ile ya kuni 15,000” alisema Makalla.

Aidha ameziagiza Halmashauri zote za mkoa huo na Hifadhi za taifa zote kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu na wale wanaofanya shughuli za kibinadamu kando kando ya mito kama inavyoelekeza sheria ya mita 60 na ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote kufanya tathimini na kutekeleza agizo lake.


“Pamoja na hayo niliyokwisha eleza, napenda nichukue fursa hii pia kusisitiza kuwa tuendelee kudumisha mila, utamaduni na desturi nzuri zinazolenga kuamsha ari ya upandaji na utunzaji miti na kuchochea uendelezaji na uhifadhi wa mazingira” alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wa sekretarieti ya utekelezaji wa mpango wa hifadhi wa safu za mlima Mbeya, ilimweleza mkuu wa mkoa huyo kuwa pamoja na kuendelea vizuri na kazi zao, wanakabiliwa na baadhi ya changamoto.

“Kubwa ni uharibifu kwenye vyanzo vya maji unaosababisha kuongezeka kwa tope kwenye vyanzo vya maji hasa kipindi hiki cha masika na hivyo huongeza sana gharama za kusafisha na kutibu maji” alisema Joseph Butuyuyu kwa niaba ya sekretarieti hiyo.

Changamoto nyingine walisema ni Taasisi nyingi za serikali kutolipia Ankara zao kwa wakati ambapo mpaka leo walikuwa wanazidai taasisi hizo za serikali maduhuri ya zaidi ya Tshs Bilioni moja na nusu.

Akizungumza na blog hii katika siku hiyo ya kilele cha Mazingira, ofisa habari wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Mbeya Neema Stantoni, alisema mpaka kufikia leo wamepanda miti 31,350 na kugawia taasisi za Afya na elimu miche ya matunda.

“Lengo kubwa ni kuwahimiza wananchi kutokata miti katika hifadhi ya vyanzo vya maji” alisema Neema.

No comments: