Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, January 29, 2017

SAUTI KUTOKA NYIKANI; MAGUFULI WALIO WAKE ANAWAJUA

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli


Na Gordon Kalulunga


WALIOPASUA barabara ambazo kwa sasa tunapita kirahisi walifanya kazi ngumu sana ya kupasua miamba na kukata mizizi ya miti kisha kuanza kusogeza kokoto na lami.


Maandalizi ya anayeendesha gari ni tofauti sana na maandalizi ya
kutengeneza barabara na hapo ikumbukwe kuwa hamuwezi kufanana hata kidogo, lazima upande mmoja uwe na uvumilivu zaidi.


Hata katika maandiko matakatifu tunaambiwa kuwa Ibrahimu hakurithi
ahadi kwa imani bali alilithi kwa imani na uvumilivu.


Mungu akikupa imani pia aachi kukupa uvumilivu. Riziki kama imepangwa na yeye ujue kuwa lazima ije tu, kikubwa ni imani na uvumilivu maana hata kama unahitaji kifaranga lazima yai liatamiwe siku 24 ndipo kifaranga kitotolewe.


Mtu yeyote anayejua siri iliyopo ndani ya yai huwa hapasui yai kabla
halijaatamiwa siku hizo na akipasua yai kabla ya siku hizo kutimia
wakati wa kuatamiwa basi anakuwa na uhakika kuwa hatopata kifaranga na anaharibu matokeo.


Hakuna mtu yeyote mwenye maono halafu akawa na hasira za kipumbavu maana mwenye maono ana imani na uvumilivu.


Katika kitabu cha Isaya 1;16-18 inasema jiosheni, jitakaseni, ondoeni
uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabayajifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki, wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya njooni, tusemezane asema Bwana. Dhambi zenu zijapokua nyekundu sana, zitakua nyeupe kama theluji; zijapokua nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufi.


Huo hapo juu ulikuwa ni utangulizi wa salamu zangu kwenu maana ni muda wa miezi sita sasa tangu nitoweke katika ukurasa huu wa Sauti kutoka Nyikani, sasa nimerejea.


Februari 5 mwaka huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake na hapo ndipo ninapoanzia.


Wakati chama hicho kinatimiza miaka hiyo baadhi ya wana CCM
wameondolewa amani na teuzi za uongozi zinazofanywa na mwenyekiti wao ngazi ya taifa rais Dkt. John Magufuli.


Baadhi yao tena viongozi wamekuwa wakinung’unikia teuzi za Mawaziri na wabunge ikiwemo nafasi ya Prof. John Aidan Mwaluko Kabudi Palamagamba, uteuzi wa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole na baadhi za ajira za ukurugenzi, ukuu wa wilaya na ajira ndani ya jumuiya za chama hicho.


Wameendelea kuhojiana kuwa ni “wapiganaji” wangapi ambao wametukanwa, wamedharauliwa, wamechafuliwa, wameumizwa, wamepoteza mali zao na hata ndugu zao wakipambania chama hicho kwa muda mrefu lakini hawaonywi.


Mioyo yao inasikitika kuwa kumbe kupigania chama hicho si lolote wala chochote maana kila baada ya uchaguzi teuzi za kwenda kulia kivulini wanapewa watu ambao hawajawahi kuonekana katika uwanja wa mapambano.


Baadhi huku Nyikani wamekata tamaa hata kuwania nafasi ndani ya chama hicho mwaka huu katika uchaguzi ambao unaanza mwezi huu katika ngazi ya mashina na matawi.


Wanachama hao wakiwemo vijana, mioyo yao haina amani tena ya kuendelea kukipigania chama chao kwasababu wanaona ndoto zao hazitimii.
No comments: