Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, January 19, 2017

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2017.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama katika kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii, wanaheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na tukio 01 la ajali ya vifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 18.01.2017 majira ya saa 20:30 usiku huko Kijiji cha Kongolo – Mswiswi, Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za usajili T.348 DEK aina ya Mitsubishi Fuso likiendeshwa na Dereva aitwaye DEO MGAYA [25] Mkazi wa Mbeya liligongana na Gari lenye namba za usajili T.321 DAK aina ya Nissan Diesel Basi Mali ya Kampuni ya Taqwa lililokuwa likiendeshwa na Dereva aitwaye HAMIS HASSAN [62] Mkazi wa Dar es Salaam lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Lubumbashi Nchini Kongo na kupoteza uelekeo na kugonga Gari nyingine yenye namba za usajili T.143 BUK lenye Tela T.911 BXN aina ya Leyland DAF lililokuwa likiendeshwa na Dereva aitwaye BURHANI SULEIMAN [42] Mkazi wa Chimala na kusababisha vifo vya watu watatu.

Watu waliofariki katika ajali hiyo ni 1. HAMZA IBRAHIM ambaye alikuwa Dereva Msaidizi wa Gari lenye namba za usajili T.321 DAK aina ya Nissan Diesel Basi 2. SHIZYA HONJAS [24] ambaye alikuwa Dereva Msaidizi wa Gari lenye namba za usajili T.348 DEK aina ya Mitsubishi Fuso na 3. Mwanamke mmoja ambaye bado hajatambuliwa.

Aidha katika ajali hiyo watu 16 walipata majeraha, majeruhi 08 walitibiwa na kuruhusiwa na majeruhi 08 wamelazwa katika Hospitali ya Mission Chimala kati yao 07 ni wanaume na 01 ni mwanamke ambao ni 1. HUSSEIN MWANJALI [51] Mkazi wa DSM 2. ADEN JASON MWAMBANDE [32] Mkazi wa Kyela 3. SHABANI ALLY [30] Mkazi wa DSM 4. KAPINGA DOMINICK [32] Mkazi wa Afrika Kusini.

Majeruhi wengine waliolazwa ni 5. SHABANI MOHAMED [36] Mkazi wa DSM 6. LUGANO HAKSON [27] Mkazi wa Mbalizi Mbeya 7. LUYAMBA MHUMBI MALYETI [45] Mkazi wa Lubumbashi – Kongo na 8. KALENGA KABANGE [39] Mkazi wa Kongo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva Gari yenye namba za usajili T.348 DEK aina ya Mitsubishi Fuso kutaka kulipita Gari la mbele yake bila kuchukua tahadhari na mwendo kasi wa Dereva wa Basi.

WITO:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini ikiwa ni pamoja na kufuata sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.


                                                 Imesainiwa na:
[EMANUEL G. LUKULA - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: