Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, February 03, 2017

BREAKING: BINTI WA MIAKA 21 AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA MBEYA

Taarifa zilizotufikia muda huu kutoka Nyikani ni kwamba binti Anitha Abel mwenye miaka 21 mkazi wa Mapelele kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya mkoani humo amekamatwa na kete 15 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Mpaka muda huu yupo kituo cha Polisi kanda maalum ya kipolisi Mbalizi.

Amekamatwa majira ya SAA tano asubuhi...

Nitawajuza zaidi maana nipo juu ya mti na kikosi kazi chetu maarufu kama Quickly Response Unit tayari kimetega antena zake.

Binti huyo ni mmoja wa watoto wa mmoja wa wanawake wanaotajwa kuwa ni Mataukuni wa Biashara hiyo ambao miaka ya hivi karibuni wamepelekea mmoja wa askari Mgambo wa kituo hicho cha Polisi kufukuzwa kibarua baada ya kugusa nyayo za baadhi ya wakubwa zake kwa kumwendea mwana mama huyo na kuchukua pesa ya chai kwa kutumia jina la mmoja wa askari aliyekuwepo kituoni hapo.

Zaidi endelea kututembelea katika blog hii ya www.kalulunga.blogspot.com

No comments: