Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, February 24, 2017

CHUNYA WAJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO WA WAFUNGWA
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

WILAYA ya Chunya mkoani Mbeya imeanza ujenzi wa Gereza la Wilaya litakaloondoa adha ya msongamano wa mahabusu katika Gereza la Ruanda na kuchelewa kwa kesi kutokana na ukosefu wa Gereza.

Mkuu wa Wilaya hiyo Rehema Madusa amesema hivi sasa ujenzi wa Gereza hilo lenye eneo la ekari 165 litakuwa na Gereza, Nyumba za Askari, mashamba ya kilimo, mifugo na ufundi.

Madusa amesema shughuli za ujenzi huo zinafadhiwa na Mdau wa maendeleo Merhab Abdullahabu ambaye atakamilisha katika kipindi kisichozidi miezi sita.

Amesema kukamilika kwa Gereza hilo kutawaondolea adha wananchi ambao wanakuwa na kesi mahakamani lakini kesi kuchelewa kutokana na mahabusu wao kuhifadhiwa Gereza la Ruanda Mbeya na wakati mwingine Polisi kukosa gari au mafuta ya gari.

Hali hiyo imekuwa kero kubwa kwa wananchi na wakazi hao hivyo kukamilika kwa Gereza kutasaidia kuondoa msongamano usio wa lazima katika Gereza la Ruanda.

Aidha amesema baada ya kukamilika kwa kambi hiyo kutasaidia kuanza ufyatuaji wa tofali kwa ajili ya ujenzi wa Gereza na kuanza kuhifadhi mahabusu badala ya kuwapeleka Mbeya kama ilivyo sasa.

No comments: