Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, February 16, 2017

DAWA ZA KULEVYA ZATIKISA MBEYA, WABABE NAO WAKAMATWA

OPARESHENI ya kukamata watuhumiwa wa dawa za kulevya nchini Tanzania, imeendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoani Mbeya ambako baadhi ya wafanyabiashara wamekamatwa wakihusishwa na biashara hiyo.

Mmoja wa wafanyabiashara hao ametajwa kwa jina la Steven ambaye ni mmiliki wa maduka ya dawa za binadamu maarufu kama Maranatha.

Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimeeleza kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwanzoni mwa wiki hii na kikosi maalum ambacho hakikuhusisha askari wa jeshi hilo mkoani Mbeya.

hata hivyo, tayari baadhi ya wafanyabiashara wenine ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kujihusisha katika uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya Jijini Mbeya na nje ya vitongoji vyake wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka Mbalizi, Mama John na Uyole.

Maeneo hayo ya Mbalizi, Mama John na Uyole ni maeneo ambayo yanatajwa kuwa na wauzaji wakubwa ambao hapo awali walikuwa hawagusiki kirahisi na baadhi ya wanaostahili kushughulika na wahalifu.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na Roda Mwambera, Shaban Ramadhani, Mrisho Ramadhani na Mussa Kimbe.

No comments: