Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, February 24, 2017

DC CHUNYA AKWAZWA NA MAAFISA USTAWI JAMII WASIO WAADILIFU

Na, Ezekiel Kamanga, Mbeya

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Rehema Madusa amesema kuwa vitendo vya uhalifu katika Wilaya yake havina nafasi kwani amejipanga kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Ameyasema hayo ofisini kwake baada ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi waliolalamikia namna wanavyoachiliwa watu waliofungwa kwa makosa ya jinai yakiwemo ya ubakaji na kuwaacha wenye makosa madogo wakitumikia vifungo Magereza.

Madusa amesema Maafisa Ustawi wa jamii Wilaya na Mkoa wamechangia kwa kiasi kikubwa malamiko hayo kutokana na mmoja ya wa watu aliyefungwa kwa kosa la ubakaji kuachiwa huru baada ya maafisa hao kutoa barua ya msamaha kwa mfungwa huyo.

Aidha amesema kuwa anafuatilia namna mtu huyo alivyopewa msamaha na kama taratibu zilikiukwa mfungwa huyo akarudishwa gerezani kutumikia kifungo na maafisa hao watachukuliwa hatua za kinidhamu ili kukomesha vitendo vya uhalifu katika Wilaya ya Chunya.

Hata hivyo hivyo Wilaya ya Chunya ni moja ya Wilaya zinazokabiliwa na vitendo vya ubakaji na wizi wa kutumia nguvu lakini pamoja na Jeshi la Polisi na Mahakama kukabiliana na vitendo hivyo lakini sasa idara ya ustawi wa jamii imeonekana kukinzana na vitendo vya uhalifu.

No comments: