Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, February 26, 2017

MADIWANI SONGWE WAMKATAA MTEULE WA MAGUFULI


* Atuhumiwa pia kujimilikisha Hekali zaidi ya 200 kwa muda mfupi

* Wamwambia asikanyage ofisini mpaka atakaponyakuliwa na aliyemteua

Na Gordon Kalulunga, Songwe

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani hapa (wamemfukuza) katika Halmashauri hiyo Mkurugenzi Mtendaji Elius Nawera kwa tuhuma za kutoridhishwa na utendaji wake.

Azimio hilo liliafikiwa juzi na madiwani 23 waliohudhuria baraza hilo la dharula baada ya kusomwa taarifa ya kamati ya mipango na fedha na Mwenyekiti wao Ibrahim Sambila, ndani ya ukumbi wa Halmashauri hiyo.Mwenyekiti huyo alisema  Mkurugenzi huyo tangu Halmashauri yao iundwe Septemba 15, 2016 ameshindwa kutekeleza maazimio mbali mbali anayoagizwa na Baraza la madiwani pamoja na kukosa ushirikiano na Wakuu wake wa Idara na kusababisha migogoro kwa watumishi.Alisema kikao cha Kamati ya Fedha na mipango kilichoketi Oktoba 13, 2016 kilibaini mapungufu ya kiutendaji ya Mkurugenzi na uwepo wa migogoro baina ya wakuu wa Idara na watumishi hali iliyopelekea kuudhofisha halmashauri."Baada ya kikao hicho Kamati ilimuonya Mkurugenzi kuacha kusababisha migogoro ambapo aliomba radhi na kukiri kutorudia tena lakini hali hiyo ilijitokeza tena katika kikao cha Novemba 15,2016 na ndipo Kamati iliamua kumhoji mtumishi mmoja mmoja" alisema Sambila.Alilieleza Baraza hilo kuwa baada ya kuwahoji watumishi wote akiwemo Mkurugenzi ilibainika kuwa asilimia 90 ya migogoro inasababishwa na Mkurugenzi huku asilimia 10 ikisababishwa na Afisa Utumishi wa Halmashauri ambapo alisema Kamati iliwapa onyo kali na wao kukiri kwa maandishi.

"Kikao cha Kamati ya Fedha na mipango kilichoketi Disemba 12,2016 kilipokea taarifa ya kubomoka kwa daraja la Kikamba na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya baadhi ya vijiji na kuharibika kwa barabara ya Galula""Kikao kilikubaliana na kumuagiza Mkurugenzi kuandika barua kwenda ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Songwe kuomba kubadilisha vifungu ili kupata fedha za kutengeneza miundombinu kwa fedha za dharula lakini hakufanya hivyo mpaka ajali imetokea na kusababisha majeruhi sita katika barabara ya Galula ambapo pia wakazi wa kata ya Gua kuishi kisiwani kutokana na daraja la Kikumba kutotengenezwa" alisema Mwenyekiti huyo.Taarifa hiyo ilieleza kwamba Mkurugenzi alifanya kikao cha Watumishi (CMT) kwa lengo la kuchagua waliokuwa wakikaimu idara ili baraza la madiwani liwaombee kuthibitishwa kuwa wakuu wa idara jambo ambalo lilifanyika na majina kupelekwa kwa Madiwani na kuyapitisha.


Baada ya kupitisha majina hayo, alisema Mkurugenzi aliandika barua kwenda kwa Katibu Tawala wa mkoa Novemba 22, 2016 akiomba kubadilishiwa majina hayo kwa madai kuwa Madiwani walimlazimisha kuchagua watumishi hao."Kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni wa kubadili maazimio ya Baraza na ni uchonganishi, jambo linalopelekea kuzolotesha maendeleo ya Wilaya.Aliongeza kuwa Kamati ya Fedha aliagiza kujengwa kwa karakana ya ufundi magari katika maeneo ya Halmashauri ili kupunguza gharama zinazopelekea magari kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matengenezo lakini jambo hilo halijatekelezwa hadi sasa.Alisema pia Mkurugenzi aliomba kibali cha kuajiri wahudumu 3 na Madereva 3 kutoka kwenye kamati jambo ambalo alikubaliwa lakini hakufuata utaratibu wa ajira ambapo alitafuta madereva kinyemela kisha kuwakabidhi magari mapya ambayo yote yameangushwa na hajatoa taarifa yoyote.Wakichangia hoja hiyo baadhi ya Madiwani wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Songwe(CCM), Philipo Mulugo walisema Mkurugenzi ameshindwa kuwaunganisha watumishi na amekuwa akikaimisha ofisi mara kwa mara.Walisema Mkurugenzi hana ushirikiano na ofisi ya Mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkuu wa Wilaya jambo linalohatarisha ustawi wa Halmashauri hiyo.Mbunge Mulugo alisema Baraza haligusi Ukurugenzi wake wala mamlaka iliyomteua bali hawako tayari kufanya nae kazi hivyo ahamishwe na kupangiwa sehemu nyingine.“Ieleweke wazi kuwa hatugusi Ukurugenzi wake bali hatuko tayari kufanya nae kazi wakupeleke sehemu nyingine Baba, sisi watuletee Mkurugenzi ambaye anaweza kuendana na kasi yetu” alisisitiza Mbunge.


Aidha Mbunge huyo alimuhoji Mkurugenzi huyo kuwa kapataje utajiri wa Hekali zaidi ya 200 ndani ya miezi isiyo zidi sita na kwamba kwanini anawakatalia wawekezaji kuwekeza katika Halmashauri hiyo hasa wanaokataa kumnufaisha yeye binafsi katika miradi wanayotaka kuwekeza? Maswali yaliyoonesha kumshitua na kumduwaza kiongozi huyo.


Madiwani hao akiwemo diwani wa Kata ya Magamba Kapala Chakupewa Makelele ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chunya, walisema Mkurugenzi huyo hakushiriki kikao cha kupitisha bajeti hivyo hadi sasa haijui bajeti ya Halmashauri na ameendelea kukaidi agizo la Rais la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na kusafirisha Madawati yaliyotolewa na Wizara ya Ulinzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo alipopewa nafasi ya kujitetea alipinga tuhuma hizo na kwamba anaonewa kwani yeye hafanyi kazi za siasa bali anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

"Hatuwezi kufanya kazi kwa umwamba huu, mimi nipo hapa kutumikia wananchi na nitaendelea maana nyie nawashauri hamshauriki" alisema Mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni Mwanasheria.

Mpaka mwisho wa Baraza hilo ambalo lilianza saa saba na dakika 35 na kumalizika saa Nane na dakika 59 mchana, madiwani waliazimia pia kuwa Mkurugenzi huyo akitoka katika ukumbi ule kutoingia tena ofisini na kwamba ofisi hiyo inapaswa kulindwa.

No comments: