Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, February 13, 2017

RC MAKALLA AIOMBA ATCL SAFARI ZA MBEYA-MALAWI-DAR

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (wa pili kulia), akiwa na viongozi wa ATCL walipomtembelea leo ofisini kwake. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam Ntunguja.


* MKuu wa Mkoa AELEKEZA safari za kikazi kwa watumishi wa serikali  Mkoa wa Mbeya kutumia shirika la Ndege la Taifa(ATCL).

* Asema Uwanja wa   Ndege  wa kimataifa wa Songwe  Ukikamilika utakuwa  ni lango  la kuingia Tanzania kwa nchi zote za kusini mwa Afrika

Uongozi wa shirika la Ndege la Taifa( Air Tanzania) umehaidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini kote  ikiwa ni sehemu YA mikakati yake YA kibiashara.

Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti wa bodi YA ATCL Ndg Emanuel Koroso na Mtendaji Mkuu wa ATCL Eng Ladislaus Matindi walipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.

Wamewashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Mbeya na watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano wanawapa wa kutumia shirika hilo ktk Safari zao na wamewaomba kuendelea kulitumia shirika hilo ambalo limeboresha huduma zake.

Mkuu wa Mkoa amelishukuru shirika la Ndege kwa kuweka Mkoa wa Mbeya ktk Safari zake na kufanya hivyo limepunguza kero YA wananchi kukwama kusafiri kama ilivyokuwa hapo awali.

Aidha ameliomba shirika hilo kuweka ktk Mipango yake watakapopata Ndege zingine kutoa huduma kwa nchi za jirani ikiwemo Malawi na zambia kwa kupitia uwanja wa Ndege wa songwe.

No comments: