Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, February 13, 2017

SAUTI KUTOKA NYIKANI: TUUKATAE UBEPARI UCHWARA


Uvamizi.

* Mabepari wametuvamia tena.

Na Gordon Kalulunga, Tanzania

Nimefikiri kwa muda mrefu lengo na maana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya kuketi na watu tofauti walionizidi umri wakiwemo waasisi wa chama hicho nchini Tanzania, nilielekezwa kwa kina Mapinduzi gani yalilengwa.

Mapinduzi yaliyopelekea chama hicho kiitwe kina hilo ili kufikia lengo mahususi ya ndoto ya waasisi wa chama ni kuhusu Mapinduzi ya fikra baada ya kutawaliwa na mataifa makubwa duniani.

Wakafanikiwa kufikia ndoto zao za mapinduzi ya fikra kwa kiasi kikubwa, lakini wale wale waliotukandamiza kifikra wamerudi tena kwa migongo tofauti na nia yao ni ile ile kufanya ubepari na kutumiliki kiakili Waafrika.

Mpira, Game na Kubeti.

Mabepari hao wameleta michezo ya mpira, Game na kamali iitwayo kubeti, mambo haya mawili hasa mijini umekuwa ulevi mkubwa kwao.

Kuna watoto wanaacha masomo kila siku baada ya kuzidiwa na ulevi wa kibepari uitwao mchezo wa (magemu).

Vijana wengi wanashinda kwenye kamali za kibepari ziitwazo kubeti na michezo ya kuangalia mpira muda mwingi. Wamelewa chakali.

Wazungu hao wameleta ubepari uchwara huo kwa lengo la kuwapumbaza Waafrika hasa vijana kuacha kufikiria mambo ya msingi ya kufanya kazi na kufanya ubunifu bali vijana tuendelee kuwaza mambo yao huku wao wakizidi kuendelea.

Kwasasa hata hapa Tanzania, ukitaka kupata udhamini wa fedha basi andaa mambo ya kijinga ikiwemo mashindano ya kutembea uchi.

Wanafanya kila wawezalo ili vijana wa kike na kiume wa Bara LA Afrika wapumbazike na kudumaza fikra zetu za kimaendeleo.

Shime Waafrika wenzangu, tumevamiwa tena. Shituka.

Gordon Kalulunga (Development Journalist),
P.O.BOX 705-Mbeya.
Cell: 0754 440 749
Email: kalulunga2006@gmail.com

No comments: