Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, February 17, 2017

TATIZO LA MAJI LATENGAMAA MBEYA MJINI

 Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Jiji la Mbeya Injinia Simon Shauri akiwa na afisa habari wa idara hiyo Neema Stanton.(Picha na Maktaba ya Kalulunga blog)
NA KALULUNGA BLOG-MBEYA

KIKOSI kazi cha Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya, kimefanikisha kutatua tatizo la hitilafu ya mitambo iliyopelekea kutokea kukwama kwa kiasi fulani upatikanaji wa maji kwa baadhi ya wateja wa Mamlaka hiyo jijini Mbeya.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Gazeti hili Mtandao (KALULUNGA BLOG)

www.kalulunga.blogspot.com wamethibitisha kurejea huduma hiyo ambayo waliikosa takribani wiki moja.


Afisa habari wa Mamlaka hiyo ya maji iliyopo kusini mwa Tanzania Neema Stanton, amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo ambalo ameeleza kuwa lilitokana na mvua iliyonyesha Januari 31 mwaka huu.

Amesema baada ya mvua hiyo kunyesha maji yaliyotiririka (mafuriko), yaliingia kwenye mitambo (Pump) za kusukuma maji hivyo kupelekea mitambo hiyo kupata hitilafu.

"Kwa sasa tumetatua tatizo na kama kuna mteja bado hajapata maji tunamuomba awasiliane nasi au aje moja kwa moja ofisini tutamsikiliza na kutatua tatizo atakalotueleza" alisem Neema Stantoni.

No comments: