Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, February 22, 2017

UVCCM KILIMANJARO WAKOLEZA MOTO VITA DAWA ZA KULEVYA

Mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Kilimanjaro,Juma Raibu.

Na Charles Ndagulla,Moshi

MAPAMBANO dhidi ya dawa za kulevya nchini yanazidi kupamba moto huku mwitikio wa jamii ukionekana kuwa mkubwa na uungwaji  mkono tangu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuanika majina ya watumia,wasambazi wa dawa za kulevya.

Mkoani Kilimanjaro,umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), pamoja na kuunga mkono mapambano hayo, umetoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwapa ulinzi wananchi watakao waanika watuhumiwa wa mtandao huo.
 

Umoja huo umetaka jamii bila kujali itikadi za kisiasa kuunga mkono mapambano hayo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa madawa hayo yanawathiri zaidi vijana ambao ndiyo nguzo kuu katika shughuli za uzalishaji mali.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini moshi na Mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Kilimanjaro,Juma Raibu katika mkutano wake na waandishi wa habari,akiunga mkono mapambano hayo ambayo yamepewa baraka pia na Rais John Pombe Magufuli ambaye amesisiti watu wote wanaojihusha na bila kuangalia umaarufu wao wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

Mbali na kutaka wananchi wanaofichua watuhumiwa wa mtandao huo kulindwa,pia ameshauri kuongezwa nguvu mapambano dhidi ya dawa hizo katika mkoa ilinayopakana na nchi jirani ambako inaaminika kuwa maeneo hayo yamekuwa yakitumiwa na wasafrishaji wa dawa hizo kuingiza nchini.

Mwenyekiti huyo wa vijana alipongeza hatua ya Rais John Pombe Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kumtaka kamishna wa Tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini,Roggers Sianga kuongeza nguvu katika vita hiyo kwenye maeneo ya mipakani hasa mkoani Kilimanjaro ambako inaaminika kuwepo na zaidi ya njia za panya 1,000 katika wilaya za Rombo,Moshi vijijini,Mwanga na Same ambazo zimekuwa zikitumika katika kuingiza bidhaa za magendo yakiwamo madawa ya kulevya.

 Kwa upande wake,katibu wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro,Yassin Lema,alitoa rai kwa vijana kuacha kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na kuwaathiri kiafya huku akiwahimiza kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ambazo ndiyo msingi mkuu wa mafanikio katika maisha yao.

No comments: