Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, February 14, 2017

VALENTINE NA UPAGANI WA KISASA

Leo hii watu wengi duniani pote wanaikumbuka tarehe ya 14 februari kuwa ni siku ya wapendanao. Swali linakuja kuwa je, tunatambua kwa nini Valentino alitoa uhai wake siku hiyo?

Tunatakiwa tupendane kwaupendo wenye msingi katika imani kama alivyofundisha mtakatifu Valentino.

Siku ya Mtakatifu Valentino ni siku ya wapendanao katika misingi ya imani na utu.

Kwa bahati mbaya watu wengi katika maisha ya leo tunapendana katika misingi ya tamaa za kimwili na kimapato.

Leo hii kuna watu wengi wa ndoa ambao wana nyumba ndogo lakini nao wanasema eti leo ni siku yao ya wapendanao.

Ni upendo gani huo wenye nyumba kubwa na ndogo? Je, Valentino hakufa kwa kupinga jambo hilo?

Vijana wengi leo wanaishi uchumba sugu bila kufunga ndoa. Lakini wao pia wanasema eti leo ni siku yao ya wapendanao.

Ni upendo gani huo pasipo msingi wa imani. Je, valentino hakutoa uhai wake ili kuwafundisha na kuwapigania vijana wafunge ndoa takatifu?

Ni ajabu kuwa siku ya Mtakatifu Valentino uovu mwingi dhidi ya upendo ndiyo hufanyika.

Ni vema siku hii iwe kwa ajili ya kujikumbusha maana halisi ya upendo.

Na alisikitika kuona hata vijana wanakosa haki za kuuishi upendo wa ndoa. Lakini akija leo hii, mtakatifu Valentino atashindwa hata kushangaa kuona jinsi upendo ulivyogeuzwa kuwa ni starehe ya kimwili badala ya kuwa ni fadhila ya kimungu.

Na mbaya zaidi atakutana na watu wa jinsia moja (ushoga na usagaji) wanaodai eti wanapendana na wana haki ya kufunga ndoa.

Katika siku hii Mtakatifu Valentino anatukumbusha tena kuwa upendo ni fadhila ya kimungu na sio starehe ya kimwili (Usasa wa upendo wa kishetani).

No comments: