Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, March 02, 2017

ASKARI POLISI ASHUKIWA KWA MAUAJI


Muuaji wa aliyekuwa Afisa mtendaji wa Mtaa katika Jiji la Mbeya Marehemu Clementina, amepatikana na kukamatwa huko Jijini Mwanza.

Amekutwa na gari pamoja na simu mojawapo ya marehemu.

Aliyekamatwa anajulikana kwa jina la Juma na ni askari wa jeshi la polisi huko Tunduma mkoani Songwe.

Katika zoezi la kumsaka na kumkamata mtu huyo, shukrani nyingi kutoka kwa watu waliokuwa wanafahamiana na marehemu wamezielekeza kwa serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ndugu Mwigulu Nchemba ambaye kupitia IGP Mangu na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wamelifanikisha hilo.

Shukrani hizo zimeelekezwa pia kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya (RPC) Dhahiri Kidavashari kwa namna alivyokuwa sambamba na jambo hilo hadi kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

Askari toka Makao Makuu DSM wakishirikiana na askari wawili toka Mbeya wamefanikisha kumkamata mtuhumia huko Mwanza na kwamba amekiri kuwa yeye ndiye aliyemuua marehemu.

mpaka usiku huu taarifa zinaeleza kuwa tayari mtuhumiwa amesafirishwa kutoka Mwanza na kupelekwa Dar es Salaam wakijiandaa kumrejesha mkoani Mbeya ambako tukio lilitokea.

Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa jambo hilo mwanzo lilikuwa likipigwa danadana na jeshi la polisi hasa Mkoa wa Songwe ambako mtuhumiwa alikuwa akifanyia kazi huko.

Makampuni ya simu ambayo yamesaidia sana kwenye sakata hili pia yamepongezwa na kwamba mtuhumiwa huyo anatuhumiwa pia kuhusika na wizi wa magari nchini Zambia na alihamishiwa Chunya mkoani Mbeya kama kituo chake cha adhabu.

No comments: