Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, March 16, 2017

IKULU KUCHUNGUZA UFISADI TANROADS KILIMANJARO
WATUMISHI wawili wa wakala wa barabara mkoani Kilimnjaro (TANROADS), wamekali kaa la moto baada ya wakandarasi wazalendo mkoani Kilimanjaro kumwandikia barua Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakimuomba atume timu ya uchunguzi kuwachunguza watumishi hao wanaodaiwa kuwa na ukwasi usioendana na kipato chao.

Wakandarasi hao wanawatuhuma watumishi hao kujilimbikia mali
zinazotokana na kujipatia manufaa kupitia  zabuni zinazoombwa na
wakandarasi ambako wamekuwa wakipewa rushwa ili kupendelea baadhi ya kampuni ambazo wana maslahi nazo.

Malalamiko ya wakadarasi hao yamo kwenye barua yao ya Februari 28 mwaka huu ambayo  nakala yake tumeiona na kuisoma, wanadai kuwa vitendo vya wakandarasi kudaiwa kutoa rushwa ya aslimia 10 pale
wanapoomba zabuni yoyote limekuwa sugu.

Wameeleza kuwa ili zabuni ikubaliwe katika mradi wenye thamani ya
shilingi Milioni 800, sharti utoe 10% ambayo ni sawa na shilingi Milioni 80 na mradi wenye thamani ya sh, Milioni 200,mzabuni sharti atoe rushwa  ya kati ya sh,Milioni 10 hadi 15.

Watumishi hao pia wanadaiwa kuwa vinara wa kuvujisha  siri za zabuni
kwa lengo la kuziwezesha kampuni ambazo wanamaslahi nazo ili ziweze
kuomba zabuni kwa kuweka kiwango cha chini kulingana na tahmani ya
mradi.

Tuhuma nyingine zilizoelekezwa kwa maofisa hao ni pamoja na kuingilia
mapendekezo ya “Evaluetion Tearm”na kubadili mapendekezo yao na
kuamuru zipewe kampuni ambazo wanamaslahi nazo.

Meneja wa Tanroads mkoa wa Kilimanjaro, Nkolante Ntije, amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo lakini akadai kuwa wakandarasi hao si wakweli kwani maammuzi ya kutoa zabuni kwa wakandarasi hayatolewi na mtu mmoja bali zipo bodi Nne zenye wajibu wa kupitia zabuni za wazabuni kabla ya kutoa mapendekezo na hatimaye kuzipa kandarasi.

“Evaluation Team si watu wa mwisho katika kutoa maamuzi ya nani apewe zabuni na nani anyimwe, tunazo bodi nne ambazo ni kitengo cha
manunuzi(PMU),bodi ya zabuni ya mkoa na meneja mwenyewe wa mkoa ambaye ndiye accounting officer”,anasema.

Wakandasi hao wanadai kuwa,ipo kampuni(wanaitaja)ambayo
haikupendekezwa Evaluation Team baada ya kubainika kuwa haikuwa na sifa lakini kutokana na kuwa na mahusiano ya karibu na mkuu wa kitengo cha manunuzi,mapendekezo ya timu hiyo yakatupwa na kampuni hiyo ikapewa kandarasi ya kujenga madaraka katika eneo la KIA na kifaru .

Kilichotokea kwa mujibu wa wakandarasi hao ni kampuni hiyo kushindwa kutekeleza mradi huo kama iliyoomba na sasa serikali inaingia gharama ya kutangaza zabuni upya.

Meneja huyo wa mkoa amekiri kampuni hiyo kupewa kandarasi na kushindwa kutekeleza mradi huo lakini akaitetea kwamba mradi ambao
kampuni hiyo imeshindwa ni mdogo ikilinganishwa na mradi mikubwa
iliyoutekeleza wilayani same.

“Ni kweli hiyo kampuni imeshindwa kujenga hayo madaraja kama
ilivyoomba na kushinda zabuni lakini tunashindwa kuelewa ni kwa nini
imeshindwa mradi mdogo kama huo wakati imetekeleza mradi mikubwa wa kujenga karavati kubwa wilayani same”,alisema.

Wakandarasi hao wanamuomba Rais Magufuli aagize kuundwa kwa timu ya uchunguzi ikihusisha wahandisi ili kuchunguza mfumo mzima wa utoaji wa zabuni na zabuni zote zilizobadilishwa kwa maelekezo ya maofisa hao baada ya evaluation team kutoa mapendekezo.


Pia wanaomba mamlaka za uchnguzi kufanya uchunguzi juu ya mali
wanazodaiwa kuwa nazo maofisa wawili wa wakala huo kama zinalingana na kipato chao na kama waliwahi kukopa benki yoyote zilizowawezesha kumiliki mali hizo.

Wakati hayo yote yakiendelea,wanamuomba rais kuamuru maofisa
wanotuhumiwa kwa ufisadi,kusimamishwa kazi ama kuondolewa katika
nafasi zao ili kupisha uchunguzi wakidai kuwa kuendelea kuwepo hapo
wanaweza kuvuruga uchunguzi na kuharibu baadhi ya nyaraka muhimu.


“Sisi wakandarasi wakizalendo tunaimani kubwa na utendaji kazi wako
ambao kwa mwaka mmoja uliokaa madarakani,umeonyesha dhamira ya dhati ya kutokomeza rushwa na ufisadi “,inasema barua hiyo.

Wakandarasi hao wakahitimisha barua yao kwenda kwa rais kwa kutamka kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zaidi pale watakapohitajika endapo timu ya uchunguzi itakundwa.

No comments: