Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, March 08, 2017

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI; MAJI YA KINYESI YAPAMBA JIJI LA MBEYA Maji machafu yenye kinyesi yakitiririka katika makazi ya watu mtaa wa Maendeleo kata ya Iyunga Jijini Mbeya ambayo imeelezwa kuwa ni zaidi ya kiezi mitatu adha hiyo inawakabili wakazi wa maeneo hayo.


Moja ya Chemba ya maji machafu ya Kinyesi ikiwa imezidiwa na kuendelea kutiririsha maji katika mtaa wa Maendeleo kata ya Iyunga Jijini Mbeya kama inavyoonekana na maji hayo yanasambaa katika makazi ya watu.

============================================== 


WAKATI Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kusini mwa Tanzania Amos Gabriel Makalla akifanya kila awezalo kuliweka safi Jiji la Mbeya, inaonyesha baadhi ya watendaji wa idara bado hawajaelewa dhamira yake wala ya Rais Dkt. John Magufuli kutokana na uchafu wa wazi ukiendelea kutapakaa katika viunga vya Jiji hilo.


Kikosi kazi cha Kalulunga blog kimeshuhudia maji yenye kinyesi yakitiririka katika makazi ya watu mtaa wa Maendeleo kata ya Iyunga Jijini humo huku wananchi wakiyakanyaga maji hayo wakiwemo watoto chini ya miaka 1o.


Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wananchi wa mtaa huo wamesema kuwa hali hiyo imedumu kwa zaidi ya miezi minne na sasa wao hawana mahala pa kwenda kwasababu ni wanyonge.


Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Elius Mwakyusa amesema hali hiyo tangu aingia madarakani mwaka 2014 imekuwa sugu licha ya hatua kadhaa kuzichukua ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Mamlaka husika na viongozi wa Haki za binadamu.


“Nimejitahidi sana na mpaka tulipofikia wananchi wanatamani kunipiga mawe maana tumelalamikia hali hiyo lakini tumekuwa tukipuuzwa na hata viongozi wote wa kata yetu akiwemo Ofisa Mtendaji wa Kata ndugu Kervin Mwasapile na wenzake wanafahamu tulivyohangaika nao pamoja lakini tunapuuzwa na Mamlaka husika” alisema Mwenyekiti huyo.


Kwa upande wao Mamlaka ya maji safi na taka Jijini humo wamesema wao hawana taarifa na tatizo hilo licha ya kwamba imeelezwa kuwa ni tatizo la muda mrefu.


Akizungumza na Mhariri Mkuu wa Blog hii, Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo Neema Stanton alisema kuwa yeye hana taarifa juu ya tatizo hilo lakini aliahidi kulifanyia kazi haraka.


“Hapa Mamlaka hatuna taarifa lakini kwasababu ndiyo kwanza tunapata taarifa hiyo tunalifanyia kazi na mafundi watafika eneo husika na kuwatatulia shida hiyo wananchi” alisema Neema Stanton.

No comments: