Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, March 31, 2017

NGUVU YANGU DHIDI YAO, KITABU KIPO SOKONI

NGUVU YANGU DHIDI YAO

Ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi Gordon Kalulunga ambaye ni mbobezi katika habari za uchunguzi na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania.

Ndani ya kitabu hiki unakutana na ladha au nta za Makala za uchunguzi na uchambuzi ikiwemo Dawa za kulevya na machungu kwa watoto na wajawazito, Ngazi tano za uongozi, wamerudi tena kututawala, Demokrasia inaruhusu matapeli kuongoza nchi, je wapinzani wanaweza kutawala? Shamba la Kapunga malaika aliyezikwa na wenye dhambi na Magufuli Kajinyonyoa.

Zingine ni Afya za Watanzania zimewekwa kwenye soko holela, Wasichana katika tanuru la mimba za utotoni, Wajawazito Tanzania wanavyokimbilia kujifungulia Malawi, Ninavyomkumbuka Amina Chifupa, Mioyo ya viongozi iliyoharibika inaharibu nchi na Mizimu inataka nchi yao.

Anayetaka siasa atapata ladha, Uchumi ladha ipo, Afya nta yake ipo, Uongozi na fasihi vyote vimesheheni.

Kitabu kinauzwa Tsh 10,000 tu.

Kwa mawasiliano ya kukinunua na kulipia tuwasiliane kwa simu 0754 440 749 au tuandikie kwa barua pepe kalulunga2006@gmail.com

Utatumiwa hapo ulipo.

No comments: