Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, March 16, 2017

SEBULE YA NYUMBA YA DC ILEJE YAOTA MAHINDI NA KUTOWEKAMKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Joseph Mkude, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvunja madaraja ya asili yaliyokuwa yanawasaidia wananchi kuvuka katika mto Songwe unaotenganisha nchi za Tanzania na Malawi.

Madaraja hayo ambavyo yalijengwa na kuunganishwa kwenye miti, yalikuwa katika kata za Isongole, Bupigu na Malangali, yamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa nyakati za masika mto huo unapojaa maji.

Taarifa zinasema kuwa, kiongozi huyo aliamuru madaraja hayo kuvunjwa wiki mbili zilizopita kwa madai kuwa yalikuwa yanatumika kuvusha bidhaa za magendo na biashara haramu ya dawa za kulevya.

 Baada ya kutekeleza azma yake hiyo ambayo haikuungwa mkono na wananchi wengi, alijikuta akiamka asubuhi huku sebule ya nyumba yake ikiwa imegeuka kuwa shamba la mahindi yaliyoota kwenye sakafu ya malumalu.

Hali hiyo ilimshitua na kumlazimu kwenda kuitisha mkutano wa hadhara na kuomba radhi huku akiahidi kujenga upya madaraja hayo.

Baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo waliohojiwa na KALULUNGA BLOG www.kalulunga.blogspot.com walisema uamuzi huo haukuwa sahihi na kwamba kiongozi huyo alikurupuka na kufanya maamuzi bila hata kuwa na takwimu za uhalifu aliokuwa amedai unafanyika kupitia madaraja hayo.

Mwananchi Elius Ndabila anasema Mkuu huyo wa wilaya alifanya maamuzi hayo bila kufanya utafiti shirikishi na kwamba madaraja hayo yapo tangu enzi za mababu zao.

“Kuna wamalawi wana mashamba Ileje, wanasoma Tanzania hali kadhalika watanzania wanasoma, wanalima, wanaoa na hata mambo mengine ya kimila wanashirikiana na njia pekee ya mawasiliano ni madaraja hayo” anasema Ndabila.

Anaeleza kwamba “Hatuwezi kuwalazimisha wana Ileje wote wanaotaka kwenda Malawi wakapite katika daraja la Isongole au Kasumulu ni gharama kubwa na ukisema madaraja yanatumika vibaya vipi kiangazi mto unapopungua maji, ambapo kila mahala mtu anavuka? Wakiona hivyo waongeze ulinzi” anasema Ndabila.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa kuna mkakati wa Madiwani wa kutoa tamko kuhusu uvunjaji wa madaraja hayo.

No comments: