Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, March 31, 2017

UTATA BILIONI 9 WAKWAMISHA UUZAJI VIWANJA SONGWE MBEYA

Uuzwaji wa viwanja vya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya umeingia mchanga baada ya kuwepo harufu ya ufisadi na matumizi tata ya Shilingi Bilioni 9.

Viwanja hivyo vilivyopo eneo la Viwanda, Songwe Industry Area jimbo la Mbeya Vijijini karibu na uwanja wa ndege, mpaka sasa vimeshindwa kuuzwa kutokana na baadhi ya vielelezo vya matumizi ya fedha kushindwa kuonekana.

Uchunguzi wa kikosi kazi chetu cha mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com umebaini kuwa utata huo unatokana na matumizi ya bilioni tisa ambazo zinashindwa kuthibitika.

Vyanzo vyetu vya habari vimesema matumizi hayo yameshitukiwa na madiwani wa Halmashuri hiyo ikiwemo matumizi ya shilingi Milioni 700 kwa ajili ya utawala tu.

Mbali na utawala pia imeelezwa kuwa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na kampuni iliyopewa tender ya uuzaji wa viwanja hivyo ilitoa taarifa kuwa ilitumia Shilingi Milioni 360 kwa ajili ya matangazo.

Ukwetuaji wa Barabara nao umeongeza utata kwa taarifa kuwa wametumia bilioni 2.5 wakati kipande cha Lami kilomita moja hutumia bilioni moja na jumla ya bilioni 9 inadaiwa kutumika katika maandalizi ya viwanja hivyo.

Kutokana na matumizi hayo, madiwani wamekataa kuruhusu wahitaji wa viwanja hivyo kuanza kulipa pesa kwa Mweka hazina (DT) wa Halamshauri hiyo aliyetajwa kwa jina la Mwakalasi mpaka hapo vielelezo vya matumizi ya fedha hizo vitakapopatikana.

Taarifa zinasema uongozi wa Halmashauri hiyo unaendelea kumshinikiza DT huyo kupokea fedha ambapo yeye amehitaji kuandikiwa barua ili aanze kuchukua fedha kwa wanunuzi wa viwanja hali ambayo inaleta kigugumizi.

Kutokana na msuguano huo, inadaiwa kuwa kaimu DT huyo mpaka sasa anakaimu nafasi hiyo na madiwani wamemshinikiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ameichiory Joseph kupeleka barua TAMISEMI ili atambuliwe.

No comments: