Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, March 01, 2017

WABABE WA WAJAWAZITO KITANZINI


Dar es salaam 01/03/2017

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amewataka Maafisa Kazi wote nchini kuwafuatilia waajiri wote wanaoachisha kazi wanawake wanaopata mimba wakiwa kazini.  

Aliyasema hayo leo katika Ukumbi wa Shirika la TGNP Mtandao, Mabibo Dar es salaam wakati wa mkutano uliojadili masuala ya Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unavyokuwa kikwazo katika ukombozi wa wanawake kiuchumi na kushiriki katika uongozi. Mkutano huu ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2017.

Akiongea katika mkutano huo Waziri Ummy alikemea tabia ya baadhi ya waajiri kuwafukuza kazi wanawake wanaopata mimba wakiwa kazini. Alisema, “Suala la Wanawake kubeba mimba ni haki yake ya msingi ambayo haiepukiki, inashangaza baadhi ya waajiri kuweka masharti kwa wafanyakazi wao wa jinsi ya kike kutobeba mimba mara wanapo waajiri”. Mhe Ummy alisisitiza kuwa “Huu ni Ukatili wa kijinsia ambao serikali haiwezi kuuvumilia”.

No comments: