Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, March 05, 2017

WANAHABARI MBEYA WALIOZURU KABURI LA NYERERE WAREJEAZIARA iliyowahusisha wanahabari 9 wa klabu ya waandishi wa habari Mbeya Press Club (MBPC) walioenda kutembelea Makumbusho na kuzuru kaburi la mwasisi wa Taifa la Tanzania Julius Kambarage Nyerere, imefikia tamati na wanahabari hao wamerejea salama Jijini Mbeya.Katibu wa Mbeya Press Club Emmanuel Lengwa, aliyekuwa miongoni mwa wanahabari waliofanya ziara hiyo amesema serikali na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere, wanapaswa kuketi pamoja ili kuyafanya makumbusho hayo kuwa na tija kwa pande zote mbili.


''Nimegundua, pale Mwitongo kuna miradi miwili au mitatu inayohusiana na utalii ambayo ni makumbusho ya Mwl. Nyerere ambayo yanasimamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kitengo cha Makumbusho ya Taifa"

" Pili kuna Kaburi la Baba wa Taifa, makazi yake na hata eneo zima la kuzunguka makazi ya baba wa Taifa ikiwemo makaburi ya wazazi wake na wanafamilia wengine, mradi huu unasimamiwa na familia ya Baba wa Taifa"

"Tatu ni mradi wa hotel ya kitalii ya Mwitongo unaosimamiwa na mjukuu wa Baba wa Taifa. Katika kila mradi ukienda utalipa kiingilio na haviingiliani. Nadhani miradi yote hii ingeunganishwa na wakaingia ubia (share) ungefanya vizuri zaidi kwa manufaa ya taifa'' amesema Lengwa.


Wanahabari hao ambao ni Ndugu Modest Nkulu, Asha Athuman, Kenneth Ngelesi, Meshark Njavike, Eliud Ngondo, Emmanuel Lengwa, Albert Msole, Naomi Victor na Hawa Mathias wametembea takribani kilomita 2,800 wakipitia katika mikoa ya Njombe, Iringa, Dodoma, Singida, Shinyanga na Mwanza, Simiyu na Mara  pia walipata  fursa ya kutembelea vivutio vya Utalii katika mikoa ya Singida na Mwanza.


Imeandaliwa na Kenneth Ngelesi na Kuhaririwa na Gordon Kalulunga.

No comments: