Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, March 26, 2017

WANAODHANIWA KUMUUA POLISI WAKAMATWA

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limesema linawashikilia watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya askari wake, Abdalah Chande Fakhi.

Fakhi ambaye alikuwa na cheo cha sajini aliuawa na wananchi katika eneo la KDC Msaranga mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema ingawa hawajajua chanzo cha tukio hilo, lakini wanawashikiliia watu kadhaa na wengine wanaendelea kusakwa.

 “Kwenye saa 1:30 usiku jana (juzi) tulipokea taarifa kuwa kuna raia anafukuzwa huku watu wakisema mwizi..mwizi. Polisi walikwenda hilo eneo lakini wakakuta wale watu wametawanyika,”amesema.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, mtu huyo alikuwa kwenye nyumba aliyokimbilia kwa usalama na walimchukua na kumkimbiza KCMC kwa matibabu na ndipo walipogundua kuwa ni askari.

Hata hivyo, amesema askari huyo alifariki dunia saa mbili usiku wakati madaktari na wauguzi wakijitahidi kuokoa maisha yake, na katika hali aliyokuwa nayo hakuweza kuzungumza chochote.

No comments: